Baada ya msanii wa Bongo Flava Marioo kutangaza ujio wa Album yake ya pili, hatimaye hivi leo ametangaza list ya nyimbo 17 ambazo zita patikana kwenye album yake hiyo kwa jina la “TheGodSon (TGS)”.
Tip of the Day - Music
Former President Julius Nyerere heavily influenced the music scene by promoting traditional African music and values, embedding Tanzanian identity into songs and artistic performances.
Kwenye album hii mpya, Marioo ameshirikiana na wasanii mbalimbali kutoka Afrika, akiwemo Bien kutoka Kenya, King Promise kutoka Ghana, Patoranking Kutoka Nigeria, Eleeeh Kutoka Rwanda, pamoja na Joshua Baraka kutoka Uganda. Kwa wasanii wa Tanzania, Marioo amewashirikiana na wasanii kama, Alikiba, Harmonize, Aslay na msanii chipukizi Stan kutoka Label ya Bad Nation inayomilikiwa na Marioo.
Here is the tracklist for Marioo’s album The Godson
- Alhamdulillah
- My Daughter
- Sober (feat. Alikiba)
- Nairobi (feat. Bien)
- Dar es Salaam
- Happiness (feat. Kenny Sol)
- Salio
- Wangu (feat. Harmonize)
- My Eyes (feat. Patoranking)
- Pini (feat. Aslay)
- Njozi (feat. Elleeh)
- No One (feat. King Promise)
- High (feat. Joshua Baraka)
- Why
- 2025 (feat. Stans)
- Hakuna Matata
- Unanichekesha
Album ya The Godson au TGS inatarajiwa kutoka mwezi huu wa kumi na moja, tarehe 29 siku ya ijumaa. Mbali ya Album hiyo kuwa na kolabo za wasanii wakali, pia album hii imetengenezwa na maproducer mbalimbali kama vile Kaniba, Click Master, Traxx, Eleeeh, Cukie Dady, BLVCQ, S2kizzy pamoja na Abbah. Kwa sasa unaweza ku-pre oder Album hii kupitia Mitandao Yote ya Kustream muziki.