Zuchu atavishwa pete siku ya Valentines - Mama Dangote athibitisha — citiMuzik

2 years ago By Zuchu atavishwa pete siku ya Valentines 1.6K
Are you a music lover looking for the latest track to add to your playlist? Look no further. Get ready for an unforgettable musical experience as we present a song by Zuchu atavishwa pete siku ya Valentines Mama Dangote athibitisha — citiMuzik.

Zuchu atavishwa pete siku ya Valentines Mama Dangote athibitisha — citiMuzik


Wakati tetesi kwamba mastaa wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz pamoja Zuchu wako katika mahusiano na wanapanga kufunga ndoa muda sio mrefu.

RELATED: Marafiki zangu ni Wanaume, Wanawake ni wanafiki – Irene Uwoya

Basi duru za kuaminika zimetaarifu kwamba kwa kweli jambo kubwa linaenda kutokea Bongo hivi karibuni.

Bi Sanura Kassim almaarufu kama Mama Dangote na ambaye ni mama mzazi wa Diamond amethibitisha kuwa mtunzi wa kibao ‘Sukari’ Zuhura Othman almaarufu kama Zuchu atakuwa anavishwa pete mnamo siku ya wapendanao, ukipenda Valentines.

Mama Dangote alifichua hayo kupitia mtandao wa Instagram baada ya kuulizwa iwapo ni kweli mwanawe Diamond atakuwa anafunga pingu za maisha na Zuchu.

“Eti tarehe 14 Zuchu anaoewa Mama Diamond?” Binamu ya Diamond Romy Jones alimuuliza Mama Dangote.

“Anavishwa pete” Mama Dangote alimjibu Jones.

Haya yanajiri muda mfupi tu baada ya nyota wa taarabu Khadija Kopa kufichua kwamba tarehe 14 Februari itakuwa siku kubwa kwa binti yake Zuchu.

Bi Kopa alimtakia bintiye furaha na mafanikio makubwa ifikapo siku ile huku akimhakikishia kwamba ataendelea kuunga mkono maamuzi yake.

RELATED: Mchumba hasomeshwi – Baba Levo amchana Rayvanny kuhusu Paula (+Video)

“Zuhura mwanangu Nimekulea kwenye maadili na Najua wewe ni binti mwenye maamuzi sahihi na mimi kama Mama yako niseme sina budi kukusapoti .Tarehe 14 inaenda kua siku yako kubwa hakuna mwanamke asie na ndoto hii.

M/Mungu akakusimamie najua hutoniangusha .siku hii isiwe tu siku yako kubwa duniani basi pia ikawe ndo mwanzo wa maisha mapya yenye Furaha .M/Mungu Akulinde kiziwanda changu Amin” Bi Kopa aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram

Wanamitandao wameendelea kumwandikia Zuchu jumbe za pongezi na heri njema huku wengi wakibashiri kuwa atakayekuwa anamvisha pete sio mwingine wala ni Simba mwenyewe, Diamond Platnumz.

Also, check more tracks from Zuchu;

Download Now 1.6K
Install Android App
Developer: Tanzania Tech Media
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot