Wazee Walisaidie Kanisa kupambana na Changamoto za Maisha na Utume wake

1 month ago 123
Wazee Walisaidie Kanisa kupambana na Changamoto za Maisha na Utume wake, download nyimbo mpya. Download hapa Wazee Walisaidie Kanisa kupambana na Changamoto za Maisha na Utume wake.

Baraza la Maaskofu Katoliki Malawi katika maadhimisho ya Siku ya Wazee na Wajukuu, linasema, wazee wana mang’amuzi, ujuzi, maarifa na uzoefu wa miaka mingi, walisaidie Kanisa kupambana na changamoto mamboleo katika maisha na utume wake! Kwa hakika wazee ni chemchemi ya imani, matumaini na mapendo. Wazee ni watu muhimu sana katika historia ya binadamu! Utu!

Ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko katika maadhimisho ya Siku ya Wazee na Wajukuu Duniani Jumapili tarehe 25 Julai 2021, unanogeshwa na kauli mbiu: “Na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote” Mt 28:20. Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani yatakuwa yanakaribiana sana na Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Watakatifu Joakim na Anna, wazazi wake Bikira Maria ambayo inaadhimishwa Jumatatu tarehe 26 Julai 2021.

Baba Mtakatifu anawataka mababu, mabibi na wazee kujikita katika nguzo kuu tatu za maisha: Ndoto, Kumbukumbu na Sala kama kielelezo cha uwepo endelevu wa Kristo Yesu kwa waja wake. “Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono” Yoe 2: 28-32.

Siku ya Wazee na Wajukuu Duniani ni matunda yanayobubujika kutoka katika Maadhimisho ya Mwaka wa Furaha ya Upendo Ndani ya Familia, “Famiglia Amoris Laetitia” uliozinduliwa rasmi tarehe 19 Machi 2021 na utahitimishwa wakati wa maadhimisho ya Siku ya X ya Familia Duniani hapo tarehe 26 Juni, 2022 kwa kuongozwa na kauli mbiu: “Upendo wa familia: wito na njia ya utakatifu”.

Chanzo: vaticannews

Download Now