App ya Nyimbo Mpya imekuwa hewani kwa muda mrefu kuanzia mwaka 2022 kwa kipindi chote hiki app imepakuliwa na watu zaidi ya laki moja (100k).
Kwa kipindi chote hicho mabadiliko ya sasa ndio mabadiliko makubwa kuliko mabadiliko mengine ambayo yamewahi kufanyika kwenye app hii. Natumaini mabadiliko haya yataboresha sana jinsi unavyo sikiliza na kupakua muziki kutoka Tanzania na Africa kwa ujumla.
Kupitia makala hii nitakuonyesha baadhi ya sehemu mpya kwenye app ya Nyimbo Mpya ambayo sasa ina muonekano mpya kabisa na uwezo wa kupakua nyimbo mpya pamoja na kusikiliza nyimbo ambazo tayari umesha pakua kwenye simu yako.
Muonekano Mpya
Sasa App ya nyimbo mpya inakuja na muonekano mpya ambao natumaini itakuwa rahisi kutumia kwa kila mtu utaweza kusikiliza na kupakua muziki kwa urahisi na haraka.
Sikiliza Muziki Offline
Sasa utaweza kupakua nyimbo zote na kusikiliza bila kutumia Internet ndani ya app ya Nyimbo Mpya. Sasa kupakua nyimbo bofya sehemu ya nyimbo mpya kwenye app kisha pakua nyimbo unayotaka au unaweza kutafuta kupitia sehemu ya Ku search hakikisha sehemu ya Online imechaguliwa.
Nyimbo Player
Nyimbo Mpya app sasa inakuja na Player ambayo natumaini utaipenda kwani inakupa uwezo wa kusikiliza muziki kwa urahisi na kisasa, player hii inakuja na sehemu ya Lyrics, Equalizer, na sehemu nyingi ambazo na uhakika utazipenda.
Artists, Genre, Album, Playlist na Mengine
Sasa utaweza kupangilia nyimbo zako kwenye mpangilio bora zaidi kwani Artists, Genre, Album, Playlist na Mengine yote vitajipanga vizuri zaidi na kama una pakua nyimbo kupitia nyimbompya.com basi utaweza kufurahia muonekano mzuri wa nyimbo zako zikiwa na makava yake bila kuweka logo mahali popote.
Endelea Kudownload Nyimbo Mpya
App ya Nyimbo Mpya bado inaendelea kukupa uwezo wa kudownload na kupata ujumbe wa nyimbo mpya moja kwa moja utaweza kuendelea kupakua nyimbo mpya kila siku kwa urahisi zaidi na kwa haraka kwa kubofya sehemu chache tu.
Update Nyimbo Mpya App
Kama tayari unayo app ya Nyimbo Update app yako sasa kupitia play store unaweza kubofya link hapo chini. Kama bado huna app ya Nyimbo Mpya jaribu app hii natumaini utaipenda na kuenjoy kutumia kwenye simu yako. Kama unatumia iOS toleo jipya la app ya nyimbo mpya linakuja mwezi huu endelea kutembelea nyimbompya.com kupata habari zaidi.
Tupe maoni yako kuhusu app ya nyimbo mpya kupitia Play Store, nini tuboreshe zaidi bofya hapo chini, tuna subiri maoni yako kwa hamu!.