Rais Samia Aagiza Watu Wafanye Maombi Kwa Ajili ya Mvua Nchi Nzima

1 year ago 619
Are you a music lover looking for the latest track to add to your playlist? Look no further. Get ready for an unforgettable musical experience as we present a song by Rais Samia Aagiza Watu Wafanye Maombi Kwa Ajili ya Mvua Nchi Nzima.

Rais Samia Aagiza Watu Wafanye Maombi Kwa Ajili ya Mvua Nchi Nzima


RAIS Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi kuanza maombi nchi nzima kuombea mvua kutokana na kuchelewa kunyesha kwa wiki kadhaa na kusababisha matatizo ya uzalishaji umeme na majisafi. Akizungumza katika maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Hospitali ya Kanda ya Bugando jijini Mwanza, Rais Samia amesema maombi hayo yataanzia kwenye sherehe hizo na kuelendea katika maeneo mengine. “Pale ambapo kuna viongozi wa dini, mapepo hutoweka,” amesema katika hafla hiyo ya kihistoria iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kidini. Hata hivyo, haikuchukua muda mrefu kabla ya mvua kuanza kunyesha mahali hapo.

Hii si mara ya kwanza kwa viongozi nchini kutoa wito wa maombi. Rais wa Zamani Hayati, Dk. John Magufuli aliliongoza taifa alipotangaza maombi ya siku tatu ya kukabiliana na magonjwa ya mfumo wa hewa hususani ugonjwa wa Corona wakati nchi iliposhuhudia kuibuka tena kwa maambukizi ya UVIKO-19.

Rais Samia ameeleza kuwa mgawo wa maji na umeme unaojitokeza hivi sasa katika maeneo mbalimbali nchini unatokana na sababu za kibinadamu ambazo zimetatiza mifumo ya mvua.

Alionesha matumaini kuwa mgawo huo utapungua hivi karibuni, kutokana na operesheni zinazoendelea katika baadhi ya mabonde ikiwemo Bonde la mto Ruvu. Vilevile ameagiza mamlaka kutekeleza majukumu yao kwa bidii ili kuokoa mabonde kwa kuimarisha ulinzi ili kuzuia wavamizi.

Chanzo: HabariLeo

Download Now 619