Padri Aliyenaswa Kwenye Video Akiwabusu Wasichana wa Shule Aomba Msamaha

2 years ago By Nyimbo Mpya 741
Are you a music lover looking for the latest track to add to your playlist? Look no further. Get ready for an unforgettable musical experience as we present a song by Padri Aliyenaswa Kwenye Video Akiwabusu Wasichana wa Shule Aomba Msamaha.

Padri Aliyenaswa Kwenye Video Akiwabusu Wasichana wa Shule Aomba Msamaha


Padri Baltharzzar Obeng Larbi wa Kanisa la Kianglikana nchini Ghana ambaye alinaswa kwenye video akiwabusu wasichana wa taasi ya mafunzo ya St. Monica amejutia tukio hilo.

Imefahamishwa kwamba padri huyo ameomba msamaha kwa kanisa na kwa wananchi wa Ghana kwa jumla. ” Najutia sana tukio hilo, kwangu mimi nilidhani kilikuwa kitendo cha ubinadamu cha kuwapongeza wasichana hao ambao walikuwa wanajiandaa kwenda katika mafunzo ya nyanjani,” Alisema Padri huyo.

Wasichama hao watatu aliowabusu mbele ya madhabahu walikuwa katika mwaka wao wa tatu na walikuwa wanaelekea kukamilisha masomo yao. Padri huyo vile vile amewaomba waumini wa kanisa hilo kumuweka kwenye maombi akidai kwamba anakabiliwa na kipindi kigumu tangu video yake ilipoenezwa mitandaoni.

Aidha, Baltharzzar Larbi alikiri kwamba katika hatua ya kuwapongeza wasichana hao alishindwa kujidhibiti na aliongezea hisia za kibinadamu.

Tayari usimamizi wa kanisa hilo umeunda kamati maalum kuchunguza tukio hilo na itamchukulia hatua Padri huyo iwapo alikusudia kutenda tendo hilo.

Mkuu wa dayosisi hiyo George Dawson-Ahmoah, pia alisema kanisa hilo litashughulikia namna wanafunzi hao watakavyopatiwa ushauri nasaha punde baada ya uchunguzi kukamilika.

“Kanisa limehuzunishwa na habari hizo na lingependa kusema uchunguzi umeanzishwa tayari na padri huyo atachukuliwa hatua chini ya sheria na kanuni za Kanisa la Anglikana,” ilisoma taarifa yake George Dawson-Ahmoah. Wanamitandao walighadhabishwa na tukio hilo na kutaka serikali ya Ghana kumchukulia hatua kali padri huyo, wengi wakitaja tendo hilo kuwa la kizinzi hasa kwa mtumishi wa Mungu.

Chanzo: Tuko

Download Now 741
Install Android App
Developer: Tanzania Tech Media
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot