Padre Awaomba Wazee Kuwafundisha Vijana

2 years ago By Nyimbo Mpya 806
Are you a music lover looking for the latest track to add to your playlist? Look no further. Get ready for an unforgettable musical experience as we present a song by Padre Awaomba Wazee Kuwafundisha Vijana.

Padre Awaomba Wazee Kuwafundisha Vijana


Paroko wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Arusha, Festus Mangwangi, amewaangukia wazee, akiwaomba kutoacha jukumu lao la kuwafunda vijana kuachana na matukio ya utoaji mimba, matumizi ya dawa za kulevya, ushoga na uvunjaji wa ndoa ili kupata Taifa lenye uadilifu na linalomcha Mungu.

Padri Mangwangwi, alikuwa akizungumza na wazee zaidi ya 300 katika Kanisa la Moyo Safi wa Bikira Maria. Kanisa hilo liko chini ya Parokia ya Ungalimited.

“Zamani wazee mlikuwa mnakoka moto mnatupigia hadithi watoto, lakini siku hizi tumewaachia watoto na vijana kuongozwa na luninga na matokeo yake kizazi kimekuwa cha kisasa na kuongoza kwenye matukio ya utumiaji dawa za kulevya, milungi,ushoga,uporaji, ndoa za jinsia moja na utoaji wa mimba mambo ambayo zamani hayakuwapo,”alisema.

Padri, Mangwangi, alisema chakula na ibada hiyo vimeandaliwa kwa ushirikiano na rafiki wa kanisa hilo, Fabienne Jaquement kutoka Uswizi.

Kutokana na uhitaji huo, aliwaomba wazee hao kuendelea kutoa elimu kwa vijana na kushirikiana na kanisa kuondoa changamoto hizo ambazo zinatia aibu Taifa.

“Lakini tumeona vizuri kuukaribisha mwaka mpya kwa kula chakula pamoja na wazee wetu na kuwapatia fedha kidogo kila mmoja ili watatue changamoto ndogo walizonazo,”alisema.

Aidha, alitoa mfano, akisema mwaka jana katika eneo lao la Ungalimited, vibaka walikithiri na kupora watu mbalimbali vitu vyao, jambo ambalo kila mtu alikuwa akilia.

“Sasa hawa vijana tunaona wanaenda kubaya kama mwaka jana, mmoja wao alimpora simu mama yake, akienda kwenye biashara zake hapo darajani, wakamkaba na kumuumiza.

“Kesho yake, kijana wake anamuuliza mama yake, kwa nini unachelewa kuamka. Mama anamwambia nina maumivu mwilini, jana darajani nilikumbana na vibaka, wakanikaba na kuchukua simu yangu. Kijana akasikitika na kudai ni yeye, kwamba hakujua kama ni mama.”

Baada ya maelezo hayo, mmoja wa wazee hao Raymond Msemwa, alishukuru Kanisa Katoliki na rafiki wa kanisa hilo, kwa kuwajali wazee ambao ni hazina kwa Taifa.

“Hata Rais wetu akiongea, lazima atukumbuke wazee na serikali inatupa matibabu bure. Hivyo vyema vijana wakajifunza kuheshimu wazee na kuacha kutudharau na kutamani mali zetu kama nyumba ambazo tulitafuta kwa jasho letu na baadhi wanatuombea tufe warithi, tabia mbaya sana na hii sababu ya utumiaji madawa ya kulevya ,”alisema.

Alisema vizuri sasa vijana wakamrudia Mungu na kusali ili maisha yawaendee vizuri na kuepukana na maradhi mbalimbali.

Rafiki wa kanisa hilo, Fabienne Jaquement ambaye ni raia wa Uswizi, alisema baada ya kuwasiliana na uongozi wa kanisa hilo, alishirikisha wazazi wake huko Uswizi ambao walimtumia fedha za kuandaa chakula hicho.

Chanzo: IPP Media

Download Now 806
Install Android App
Developer: Tanzania Tech Media
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot