Paroko Afunguka Mazito Msiba wa Meya Shinyanga

2 years ago By Nyimbo Mpya 949
Are you a music lover looking for the latest track to add to your playlist? Look no further. Get ready for an unforgettable musical experience as we present a song by Paroko Afunguka Mazito Msiba wa Meya Shinyanga.

Paroko Afunguka Mazito Msiba wa Meya Shinyanga


PAROKO wa Kanisa la Romani Katoliki Ngokolo Mjini Shinyanga Aldof Makandagu, amekemea tabia kwa baadhi ya wanasiasa kutopendana wao kwa wao, kuwa wanafiki, huku wakiuana kwa kusemana maneno hovyo usiku na mchana, na njia zingine zisizoeleweka.

Makandagu amebainisha hayo Jana wakati akitoa Mahubiri kwenye misa ya kumuombea marehemu David Nkulila (57) aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Shinyanga.

Amesema hakuna watu wanafiki kama wanasiasa, ambao hupendana kwenye majukwaa tu, lakini wakitoka hapo hakuna upendo na kuanza kunafikiana, huku wakisemana maneno mabaya, na kuwataka waachane na tabia hizo bali wapendane muda wote na siyo kuishi kinafki.

“Kwenye msiba huu Sura zenu hapa zinaonekana zina huzuni, lakini ndani ya mioyo yenu mnachekelea, hizo ndiyo tabia za wanasiasa, hebu jaribuni kupendana muda wote, na kifo hiki kiwe kama funzo kwenu,”alisema Paroko Makandagu

Chanzo: IPP

Download Now 949
Install Android App
Developer: Tanzania Tech Media
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot