Njia 6 za Kuishinda Tamaa ya Kuangalia Picha na Video za Ngono
Ni wazi Picha za akina Dada wakiwa NUSU UCHI AU UCHI Zinawalenga Zaidi Akina Kaka.
Picha za Akina Dada Wenye NGUO ZA KULALIA TU, AMA NGUO ZA UFUKWENI, AU VITOVU WAZI, NGUO ZA KUBANA Nakadhalika Zinawalenga Akina Kaka Maana KWA NAMNA YA KAWAIDA YA KIBINADAMU, BILA NGUVU YA ZIADA [NGUVU YA KUEPUKA UOVU] Hakika HAUWEZI KUIPITA ILE PICHA Bila Kuitupia Jicho…
Inahitaji NGUVU KUBWA Kuliko NGUVU YA UHARIBIFU Iliyopo Kwenye Picha.
Na Hii NGUVU KUBWA Inapatikana Kwenye Mambo Yafuatayo:
1. MSIMAMO WAKO WA NINI KINAINGIA NDANI YAKO
Mtu Ambaye Ameamua KUMPENDEZA MUNGU Amejiwekea AINA GANI YA VITU Ambavyo Anaruhusu MACHO YAKE YATAZAME Na Kuna VITU HAWEZI KURUHUSU VICHAFUE MOYO WAKE!
Yesu Alisema, “TAA YA MWILI NI MACHO, MACHO YAKO YAKIWA SAFI [YASIPOPITISHA VITU VICHAFU] NA MWILI WAKO WOTE UTAKUWA SAFI [HAUTAWEZA KUTENDA DHAMBI KWA MWILI KAMA MACHO YAKO YAMEKAA VIZURI]”
2. MAOMBI YA KUUTIISHA MWILI
Paulo Anasema, “MIMI NAUFISHA MWILI WANGU KILA SIKU” Na Katika Galatia 5:24 Anasema, “WALE WALIO WA KRISTO WAMEUSULUBISHA MWILI NA TAMAA ZAKE MBAYA”
Akiwa Na Maana “KUNA UWEZEKANO WA KUUA MWILI WAKO KIASI KWAMBA KIPENGELE CHA TAMAA MBAYA NDANI YAKO KIKAFA”
Nakumbuka Nilipokuwa Sekondari Nilianzisha MPANGO-MKAKATI WA KUJIKWAMUA Toka KATIKA TAMAA MBAYA; Nilianza Kufunga Na Kuomba Kwa Ajili Ya Mwili Wangu KUTOWAKA TAMAA BALI UTUMIKE KWA UTUKUFU WA MUNGU.
Maana “MIILI YETU I MALI YAKE BWANA NA ITUMIKE KUMTUKUZA” (1Kor 6:16-20),
Na Hakika Niliona Matokeo Yake Ila Ilikuwa TOO MUCH Yaani Akina Dada Walikuwa “KAMA WAKAKA KWANGU”
Lakini Bado Ilikuwa Msaada Kwangu Na Ilinivusha Bila Shaka!
UKIJIWEKEA UTARATIBU WA KUMWELEZA MUNGU KUHUSU “UDHAIFU WAKO” NA KUOMBA NGUVU YA “KUUSHINDA MWILI NA TAMAA ZAKE” HASA KWA NJIA YA “MAOMBI YA KUFUNGA NA KUOMBA” HAKIKA UTAVUKA NA UTAKUWA MSHINDI!
3. USIJINAJISI KWA KU-FOLLOW, KU-LIKE MAPAGE [KURASA] ZENYE Video NA MAPICHA YA NGONO
Haya Makurasa [Pages] Yana NGUVU YA KIPEPO NYUMA YAKE [Demonic Influences], Na Yameanzishwa Na Kuasisiwa Na Watu Ambao Tayari WAMEPAGAWA NA HAYO MAROHO MACHAFU
Na Ndiyo Maana UKITAZAMA ZILE PICHA AU Video HATA KWA BAHATI MBAYA KAMA HUNA NGUVU YA MUNGU KUBWA UTAJIKUTA UNATAMANI KUENDELEA KUANGALIA NA KUANGALIA HADI IISHE AU KUANGALIA NA ZINAZOFUATA!
Hautakutana Na Shetani Na Mkia Wake Njiani Akiwa Anatembea, Anafanya Kazi Kupitia Watumishi Wake Hao Watu Wa Page Chafu, Video Za Ngono Na Magazeti Ya Udaku!
MTU AMBAYE “MOTO WA MUNGU UNAWAKA NDANI YAKE” HAWEZI KUKAZA JICHO KWA SEKUNDE 3 NZIMA AKIANGALIA PICHA, Video AU GAZETI LA UCHI AU NUSU UCHI MAANA NDANI YAKE [KUNA ROHO YA MUNGU] INAPINGANA NA KILE KILICHOKO KWENYE PICHA!!!
4. EPUKA MARAFIKI WAOVU WANAOPENDA HIZI PICHA, Video, MAGAZETI NA MAJARIDA MACHAFU YA UCHI NA NGONO.
Nikiwa Sekondari Nilikuwa Nakaa Chumba Kimoja Na Kaka Zangu Waliokuwa Kidato Cha Sita, Nilikuwa Kidato Cha Tatu Wakati Huo, Walikuwa Na Simu Zilizokuwa Na Uwezo Wa Internet Na Walikuwa Waki-Download Zile Picha Na Kujifungia Chumbani Kuzitazama.
Lakini Mara Zote Walipotaka Kufanya Hilo, Walikuwa WANANIAMBIA NIWAPISHE Maana Walijua SI WATU WA AINA MOJA, Nami Bila Hiyana Niliwapisha Maana SIKUWA NA HAMU NAZO NA DHAMIRI YANGU ILIJUA SI KITU SAHIHI KUTAZAMA LAKINI PIA; KULIKUWA NA NGUVU “YA KUCHUKIA KILE KITU” KULIKO “NGUVU YA KUTAKA KUONA KILE KITU”
Biblia Inasema, “KUMCHA MUNGU NI KUJITENGA NA UOVU” Yaani Kama Unasema UNA HOFU YA MUNGU, “USIJIINGIZE KWENYE DHAMBI NA UOVU UNAOUONA AU KUUJUA WAZIWAZI, BALI UKIMBIE/ UKWEPE”
Pia Biblia Inatwambia, “KILA ALIITAYE [ALITAJAYE] JINA LA BWANA NA AUACHE UOVU” Akiwa Na Maana “UKITAKA KUONA NGUVU YA JINA LA BWANA [YESU] MAISHANI MWAKO NA KWENYE MAISHA YA MAOMBI HAKIKISHA UNAUKWEPA UOVU” Ila Kama UNA MICHANGANYO Hakika HUTAONA NGUVU YA JINA LA YESU NA KUJIBIWA KWA MAOMBI YAKO!
Marafiki Wabovu Wana Uwezo Wa Kuharibu TABIA NA MWENENDO WAKO, Marafiki Walimshawishi Sauli Kuacha Mifugo Ili Aitoe Sadaka Ilhali Mungu Alimwagiza AUE KILA KITU; Kwa Ushauri Wao AKAPOTEZA UFALME WAKE,
Rafiki Mbaya YONADABU Alimpa UJANJA WA KIPEPO AMNONI Na Mwisho Wa Siku AKALALA NA DADA YAKE, NA KUPELEKEA KUJA KUUWAWA BAADA YA MUDA KIDOGO NA ABSALOM!
Rafiki Anayekuvuta Kwenye Mapicha Ya Ngono, Video, Kurasa, Magazeti na Majarida Ya Udaku HAKUPENDI, Anataka KUKUINGIZA KWENYE MATATIZO MAKUBWA SANA Ambayo HATAKUWEPO WAKATI UNATAPATAPA HUMO!
Wakwepe Marafiki Wa Aina Hiyo, WAOGOPE KAMA UKOMA!
5. JIWEKEE UTARATIBU UNAOELEWEKA WA KULISOMA NENO LA MUNGU
Uwe Na Utaratibu Wa Kueleweka Wa Kusoma Biblia Yako, Walau Sura 2 Au Zaidi Kwa Siku.
Unaweza Kusoma Sura 1 Asubuhi Kabla Ya Majukumu Ya Siku, Mchana Kabla Au Baada Ya Chakula Cha Mchana, Na Jioni Baada Ya Majukumu Ya Siku Nzima.
NENO LA MUNGU LINA NGUVU YA KUPANGUA MAWAZO NA MITAZAMO HASI, NA LITAPIGANA KUKUSAIDIA WAKATI WA JARIBU NA MAGUMU KULIKO YULE ASIYEKUWA NALO!
-NENO LIKIWA KWA WINGI NDANI YAKO HAUTAWEZA KUTENDA DHAMBI (Zaburi 119:11).
-NENO LIKIWA NDANI YAKO LINA UWEZO WA KUKUTAKASA (Yohana 17:17).
-NENO LIKIWA NDANI YAKO LITAKUWA SILAHA YA VITA UTAKAYOITUMIA KUANGUSHA KILA WAZO NA FIKIRA MBAYA NDANI YAKO [Waebrania 4:12, Waefeso 6:17, 2Kor 10:3-5).
6. UWE NA MUDA WA KUONGEZA MAARIFA NA UFAHAMU WAKO [PERSONAL DEVELOPMENT]
Walau Saa 1 Hadi Matatu Ya Siku Yako Yatumie KUINGIZA KITU KIPYA KICHWANI MWAKO.
Hakikisha UNAJUA MAMBO MENGI KADRI UWEZAVYO.
Soma Vitabu, Google, Wikipedia, Semina Za Uchumi, Motivation, Inspirations, Tembelea Watu Waliofanikiwa Katika Jambo Fulani, Kaa Nao, Wasikilize, Jifunze Kwao, Ulizia Mbinu Zao Nakadhalika.
Soma Vitabu Vya Maswala Ya FEDHA, UWEKEZAJI, UCHUMI, MASWALA MBALIMBALI YA KIROHO Mf: UCHUMI WA KIBIBLIA, MAFANIKIO KIBIBLIA, IMANI, ROHO MTAKATIFU, UTAKATIFU, UPENDO, UINJILISTI NA MENGINEYO MENGI YA KIMUNGU…
Vitabu Kuhusu MASWALA YA KIAFYA, NAMNA YA KUUTUNZA MWILI NA AFYA YAKO, MAZOEZI YA VIUNGO Nakadhalika…
Kwa Kuwa Na Muda Wa Kujiendeleza [PERSONAL DEVELOPMENT] Unaongeza UBORA NA UFANISI WA MAISHA YAKO YA SASA NA YA KESHO…
WATU WANAOISHI MAISHA YA MAFANIKIO HAPA DUNIANI, NI WATU WANAOJUA VITU VINGI SANA; WATU WASIOKUWA NA TAARIFA ZA KUTOSHA [WAJINGA] NI WATUMWA WA WENYE MAARIFA!
Mungu Anaongea Siku Zote,
Swala Ni Je, UKIISIKIA SAUTI YAKE, UNAUFANYA MOYO WAKO MGUMU?
Kumbuka, “ASHUPAZAYE SHINGO YAKE ATAVUNJIKA GHAFLA NA HAKIKA HATAPATA DAWA”
Laiti Na Sisi Tulipokuwa Tunakua Tungepata Watu Wa Kutusaidia Hivi, Kama Mungu Anavyokusaidia Wewe Kupitia Mimi, Itumie Hii Neema Vizuri, Barikiwa!