Nigeria: Pasta Azindua Chupi na Sidiria Zenye Picha Yake Kuwasaidia Wasichana na Wanawake Walio Singo Kupata Waume wa Kuwaoa
Pasta Dr J.S. Yusuf wa Kanisa la Touch for Recovery Outreach International mjini Abuja nchini Nigeria amezindua nguo za ndani na sidiria zenye chapa ya picha yake ili kuwasaidia wanawake walio singo na wanaotamani kuolewa.
Kwa mujibu wa pasta Dr J.S. Yusuf, aliagizwa na Mungu kuzindua chupi hizo za ‘baraka’ ili kufungua milango ya ndoa katika Mwaka huu Mpya.
Mchungaji huyo alinukuu mstari kwenye kitabu cha Hesabu 23:20 unaosema“Tazama nimepokea amri ya kubariki, naye amebariki, wala siwezi kubadili.”
Chupi hizo zinasemekana pia kuwasaidia wanawake kujikinga na magonjwa na kupata bahati njema wakiwa na wanaume.
Chanzo: TUKO