Kuhani Azua Taharuki Akibusu Wanafunzi wa Kike Madhabahuni

2 years ago By Nyimbo Mpya 912
Are you a music lover looking for the latest track to add to your playlist? Look no further. Get ready for an unforgettable musical experience as we present a song by Kuhani Azua Taharuki Akibusu Wanafunzi wa Kike Madhabahuni.

Kuhani Azua Taharuki Akibusu Wanafunzi wa Kike Madhabahuni


Kuhani mmoja nchini Ghana amezua taharuki baada ya picha ya video kusambaa ikimuonyesha akiwabusu wanafunzi wa kike wakati ibada ikiendelea kanisani.

Kipande cha video ambacho kimesambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo Twitter kinamuonyesha Kuhani Obeng Larbi wa Kanisa la Anglikana, akinyoosha kichwa chake kwenye mimbari(madhabahu) na kuwabusu mabinti hao mdomoni mwao, mmoja baada ya mwingine, huku waumini wakiendelea kupiga kelele.

Tukio hilo lilitokea Jumapili iliyopita katika Chuo cha St. Monica’s College of Education katika mkoa wa Ashanti nchini Ghana.

Tovuti ya habari ya Ghana, Star FM, ilimnukuu mwanafunzi mmoja wa kike wa chuo hicho akisema kwamba wakuu wa shule walikuwa wakimtafuta mwanafunzi huyo ambaye alirekodi na kushare kipande hicho cha video.

Mwanafunzi huyo ambaye hakutajwa jina alisema Mchungaji huyo alikuwa akiwabusu wanafunzi kama “onyesho la shukrani”, Japo Ripoti hiyo haikutaja kile kuhani alikuwa akiwashukuru wanafunzi hao.

“Huyo baba anayewabusu wanafunzi katika hiyo video hakujua kuwa tutashare hiyo video, Hatukuwa sawa na hali hiyo, ndiyo sababu tulikuwa tukipiga kelele. Hii ni mara ya kwanza kufanya hivi. Alimpiga busu mwanafunzi kiongozi wa shule na kisha akafanya vivyo hivyo kwa wasomaji watatu wa kike wa Biblia. Msichana wa tatu ambaye baba alimbusu ni bikira na ndiyo sababu alimpa baba shavu ili abusu lakini baba alilazimisha na kubusu midomo yake. ”

Kanisa la Anglikana nchini Ghana limesema “wamehuzunishwa” na tukio hilo.

“Kanisa limehuzunishwa na habari hiyo na linataka kusema wazi kwamba uchunguzi kamili umeanzishwa mara moja juu ya jambo hilo na Padri huyo atashughulikiwa kulingana na kanuni na maadili ya Ushirika wa Anglikana,” kanisa lilisema katika taarifa yake Jumanne.

Chanzo: PremiumtimesNG

Download Now 912
Install Android App
Developer: Tanzania Tech Media
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot