Kenya: Godfrey Siundu Padri wa Kanisa Katoliki Aliyeaga Useja na Kumuoa Mtawa

3 years ago By Nyimbo Mpya 779
Are you a music lover looking for the latest track to add to your playlist? Look no further. Get ready for an unforgettable musical experience as we present a song by Kenya: Godfrey Siundu Padri wa Kanisa Katoliki Aliyeaga Useja na Kumuoa Mtawa.

Kenya: Godfrey Siundu Padri wa Kanisa Katoliki Aliyeaga Useja na Kumuoa Mtawa


Miaka 15 iliyopita, Godfrey Siundu aliamua kuaga useja katika Kanisa Katoliki na kumuoa mpenzi wa maisha yake ambaye alikuwa mtawa.

Siundu aliondoka Kanisa Katoliki na kuanzisha Kanisa la kikatoliki la Ecumenical of Christ ambalo alisema alilifanyia mabadiliko ambayo aliongozwa na Roho Mtakatifu.

Akizungumza na TV47, mtumishi huyo wa Mungu ambaye ni baba wa watoto watatu alisema hakuna
hata mshirika mmoja wa kanisa lake alimhukumu kwa sababu ya kuacha utumishi ndani ya kanisa katoliki na kuamua kuoa.

“Baada ya kuondoka Kanisa Katoliki la Roma, nilikaa kwa muda kabla ya kuongoza misa lakini wakati
wa siku ya kuzaliwa kwa mke wangu, niliamua kuongoza misa na Roho Mtakatifu aliniambia kuwa niwaambie
watu waliokuwa wamekusanyaka mahali pale kuwa nitaanza kuongoza ibada na kuanzisha kanisa lenye
mabadiliko,” alisema.

Tangu achukue hatua hiyo, maaskofu wengine 50 wa kikatoliki walifuata nyayo zake na kuamini kuwa ni vyema mtu kutafuta ubavu wake. Alisema kuwa Papa Francis anatakiwa kurekebisha sheria ya useja na kuwaruhusu mapadri wa Katoliki kuwa na uhuru wa kuoa au la.

“Tangu nimuoe mke wangu, huwa ninakuwa na furaha kila asubuhi na familia yangu imenifanya kuridhika zaidi,” alisema. Siundu ni baba wa mabinti watatu ambao aliwazaa pamoja na mtawa ambaye sasa ni mke wake.

Kwa upande wake Stellah Siundu, mume wake amemsaidia kukua kiroho akikumbuka namna zaidi ya muongo mmoja askofu huyo alipomuambia kuwa wataoana na kweli alitimiza maneno yake.

“Jioni hiyo aliniambia, siku moja nitakuoa. Hata hakuniambia ananipenda ama ananitaka, Alisema tu atanioa,” alisema Stella.

Chanzo: TUKO

Download Now 779
Install Android App
Developer: Tanzania Tech Media
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot