JANET OTIENO AOMBOLEZA KUFUATIA KIFO CHA BABA YAKE
Top Stories
Published on June 4, 2021
Mwanamuziki maarufu wa nyimbo za injili nchini Kenya Janet Otieno pamoja na familia yake wanaomboleza kufuatia kifo cha baba yake kilichotokea Ijumaa, Juni 4, 2021.
Janet ambaye amevuma kwa kibao chake cha ‘Napokea kwako’, alitangaza kifo cha baba yake kupitia mtandao wa Instagram na tayari mashabiki wake wamemtumia salamu za pole. “Ni uchungu sana kumpoteza mzazi, moyo wangu umejaa huzuni, nisingeliwahi shuhudia wala kupitia uchungu huu, lala salama babangu, utasalia kwenye nyoyo zetu. Tafadhali kumbukeni familia yetu kwa maombi,” Janet aliandika Instagram.
Chanzo: TUKO
Click to comment