Hija ya Kitume ya Papa Francisko Nchini Iraq: Udugu wa Kibinadamu

3 years ago By Nyimbo Mpya 656
Are you a music lover looking for the latest track to add to your playlist? Look no further. Get ready for an unforgettable musical experience as we present a song by Hija ya Kitume ya Papa Francisko Nchini Iraq: Udugu wa Kibinadamu.

Hija ya Kitume ya Papa Francisko Nchini Iraq: Udugu wa Kibinadamu


Hija ya Kitume ya Papa Francisko Nchini Iraq

Hija ya kitume ya Baba Mtakatifu Francisko nchini Iraq, kuanzia Ijumaa tarehe 5 hadi Jumatatu tarehe 8 Machi 2021 imenogeshwa na kauli mbiu “Bali ninyi msiitwe Rabi, maana mwalimu wenu ni mmoja, nanyi nyote ni ndugu” Mathayo 23:8.

Hija hii ilifumbata mambo makuu matatu: Ukaribu wa Baba Mtakatifu kwa Wakristo nchini Iraq, kuhamasisha ujenzi wa Iraq mpya katika haki na usawa na kuendeleza mchakato wa majadiliano ya kidini na kiekumene ili kudumisha udugu wa kibinadamu. Baba Mtakatifu ameianza siku ya Jumatatu tarehe 8 Machi 2021 kwa Ibada ya Misa Takatifu kwenye Kikanisa cha Ubalozi wa Vatican nchini Iraq.

Ameagana na wafanyakazi, marafiki na wafadhili wa Ubalozi wa Vatican na hatimaye, akaelekea kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad. Akiwa uwanjani hapo, amekutana tena kwa faragha na viongozi wakuu wa Serikali ya Iraq. Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwenye mitandao ya kijamii anasema, Iraq itaendelea kubaki katika akili na moyo wake. Anawataka watu wa Mungu nchini Iraq kushirikiana na kushikamana kwa ajili ya ujenzi wa amani, ustawi na maendeleo ya watu wa Mungu, ili kamwe asiwepo mtu atakayeachwa nyuma.

Anapenda kuwahakikishia uwepo wake wa daima kwa njia sala na sadaka yake. Hii iwe ni fursa ya kujenga na kuimarisha mafungamano ya udugu na mshikamano katika huduma kwa ajili ya: amani, ustawi, maendeleo na mafao ya wengi.

Akiwa angani kuelekea mjini Vatican, Baba Mtakatifu amepata fursa ya kuwatumia salam na matashi mema Marais wa Iraq, Uturuki, Ugiriki, Albania na Italia. Katika ujumbe wake kwa Rais Barham Ahmed Salih Qassim wa Iraq, amemshukuru Rais kwa niaba ya familia ya watu wa Mungu nchini Iraq kwa ukarimu waliomwonesha na kumshirikisha wakati wa hija yake ya kitume nchini mwao.

Anasali na kuwaombea amani, umoja, mshikamano wa Kitaifa; ustawi na maendeleo ya watu wote wa Mungu nchini Iraq. Baba Mtakatifu katika salam zake kwa Rais Sergio Mattarella wa Italia amemwambia kwamba, anarejea tena nchini Italia kutoka katika hija yake ya kitume nchini Iraq.

Anasema, huko amebahatika kukutana na kuzungumza na Wakristo pamoja na wawakilishi wa dini mbalimbali, ambao wameshuhudia dhamana ya kutaka kuzama zaidi katika ule moyo wa kushirikishana; safari ya majadiliano, amani na utulivu. Baba Mtakatifu anamtakia heri na baraka Rais Sergio Mattarella pamoja na watu wote wa Mungu nchini Italia. Mwishoni, amewapatia baraka zake za kitume. Kwa viongozi wa nchi mbalimbali amewatakia: ustawi, maendeleo na mafao ya wengi.

Itakumbukwa kwamba, wakati Baba Mtakatifu Francisko alipokuwa akiondoka kwenda nchini Iraq, Rais Sergio Mattarella wa Italia, alimwandikia Baba Mtakatifu Francisko ujumbe wa matashi mema na pongezi, kwa kuanza tena hija zake za kitume, baada ya kusitishwa kutokana na janga la Virusi vya Korona, UVIKO-19 linaloendelea kuitesa Jumuiya ya Kimataifa.

Hii ni hija ambayo Mtakatifu Yohane Paulo II aliipania sana kutoka katika “sakafu ya moyo wake” kama sehemu ya maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 2000 ya Ukristo, lakini kwa bahati mbaya ikagonga mwamba na kushindikana kabisa. Uwepo wa Baba Mtakatifu Francisko nchini Iraq umekuwa ni chemchemi ya ushuhuda wa faraja kutoka kwa Kristo Yesu na Kanisa lake. Kimsingi Iraq na Ukanda wote wa Mashariki ya Kati ni eneo ambalo Wakristo wameteseka, wakanyanyasika na kudhulumiwa.

Kumbe, uwepo wa Baba Mtakatifu nchini Iraq umekuwa ni ushuhuda wa ukaribu na upendo wa kibaba kutoka kwa Khalifa wa Mtakatifu Petro. Hija ya kitume ya Baba Mtakatifu Francisko nchini Iraq ni sehemu ya mchakato wa majadiliano ya kidini, yaliyomwezesha kutembelea pia Umoja wa Falme za Kiarabu, UAE.

Baba Mtakatifu Francisko, kuanzia tarehe 3 hadi 5 Februari 2019, alifanya hija ya kitume ya ishirini na saba kimataifa huko Abu Dhabi, kwenye Umoja wa Falme za Kiarabu, UAE, ili kuhudhuria Mkutano wa Kimataifa wa majadiliano ya kidini ulioongozwa na kauli mbiu “Udugu wa kibinadamu”.

Baba Mtakatifu katika hija hiyo amependa kuwa ni chombo cha amani, mjenzi wa madaraja yanayowakutanisha watu ili kudumisha udugu; haki msingi, utu na heshima ya binadamu, daima uhuru wa kidini na uhuru wa kuabudu vikipewa uzito unaostahili. Rais Sergio Mattarella wa Italia anakumbushia kwamba, hija hii ya kitume ndiyo iliyozaa Hati ya Udugu wa Kibinadamu kwa Ajili ya Amani na Utulivu iliyotiwa mkwaju kati ya Baba Mtakatifu Francisko na Dr. Ahmad Al-Tayyib, Imam Mkuu wa Msikiti wa Al- Azhar, ulioko Kairo, nchini Misri, tarehe 4 Februari 2019 huko Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu.

Huu ni mwaliko kwa waamini wa dini mbali mbali duniani, kuungana na kushikamana, ili kufanya kazi katika umoja na udugu, ili kujenga na kudumisha misingi ya haki, amani na maridhiano kati ya watu. Hati hii ni nguzo msingi ya haki, amani na upatanisho. Hati inakazia pamoja na mambo mengine kwamba: binadamu wote wameumbwa kwa sura na mfano wa Mwenyezi Mungu; wanatakiwa kusimama kidete kulinda, kutunza na kudumisha: uhai wa binadamu, mazingira nyumba ya wote sanjari na kushikamana na maskini pamoja na wale wote wanaosukumizwa pembezoni mwa jamii.

Hati ya Udugu wa Kibinadamu kwa Ajili ya Amani na Utulivu inapata chimbuko lake katika mikutano elekezi iliyowasaidia waamini wa dini hizi mbili kushirikishana: furaha, majonzi, matamanio yao halali pamoja na changamoto mamboleo.

Chanzo: vaticannews.va

Download Now 656
Install Android App
Developer: Tanzania Tech Media
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot