Fahamu Njia za Kudhibiti matumizi yako ya Data Mtandaoni

3 years ago By Nyimbo Mpya 782
Are you a music lover looking for the latest track to add to your playlist? Look no further. Get ready for an unforgettable musical experience as we present a song by Fahamu Njia za Kudhibiti matumizi yako ya Data Mtandaoni.

Fahamu Njia za Kudhibiti matumizi yako ya Data Mtandaoni


Fahamu Njia za Kudhibiti matumizi yako ya Data Mtandaoni

Umeshawahi kuwa mhanga wa kifurushi chako kuisha kabla haujakusudia kiishe? Pengine umekuwa ukilalamika kuwa baadhi ya mitandao inakumalizia data zako, na hii inaweza kusababishwa na kutofahamu kiwango cha data kinachotumika kwa matumizi ya kawaida mtandaoni.

Si rahisi kuweka makadirio ya moja kwa moja ya kiwango cha data kinachotumika mtandaoni kutokana na utofauti wa matumizi ya kila mmoja, pamoja na sababu kama vile spidi ya mtandao wa intaneti unaoutumia. Lakini baada ya kufahamu makadirio ya wastani ya matumizi ya baadhi ya huduma katika mtandao wa intaneti, unaweza kupangilia hata kwa kukadiria kiasi gani cha data utakachokitumia kwa mahitaji utakakayokuwa nayo mtandaoni.

Mitandao ya Kijamii
Mitandao ya Facebook, Twitter na Instagram inatumika zaidi kutuma picha na video, lakini kadiri mitandao hiyo inavyozidi kuboreshwa, kiwango cha data kinachotumika pia kinaongezeka. Baadhi ya kampuni za mawasiliano nchini hutoa huduma ya bure kwa mitandao ya kijamii, hasa Facebook, lakini mara nyingi huduma hiyo huwa na ukomo kwenye kuona maandishi tu, si picha wala video!

Kwa wastani, mitandao ya kijamii hutumia kiwango cha MB 1.5 kwa dakika ikiwa utakuwa unapita kusoma machapisho tu, lakini pale utakapoanza kuangalia video au kutuma picha na video, kiwango hicho kinaweza kupanda hadi MB 2.6 kwa dakika. Hii inamaanisha kuwa unaweza kutumia kati ya MB 90 hadi 150 kwa saa.

Mgawanyo wa wastani wa matumizi ya data kwa baadhi ya mitandao ya kijamii unaweza kuwa:
Facebook: MB 80 kwa saa
Snapchat: MB 120 kwa saa
Twitter: MB 120 kwa saa
Instagram: MB 150 kwa saa

Unaweza kudhibiti kiwango cha matumizi ya data kwa mitandao ya kijamii kwa kubadilisha mipangilio ya matumizi kwenye programu tumishi za simu za mitandao husika. Mfano, unaweza kuzuia kuangalia video isipokuwa ikiwa kifaa chako kimeunganishwa na Wi-Fi.

Kwa Facebook, unaweza kupata mpangilio huo (kwa watumiaji wa iPhone) kwa kubonyeza alama ya mistari mitatu iliyopo upande wa kulia kisha bonyeza Settings. Chagua Account Settings > Video and Photos > Autoplay kisha chagua On Wi-Fi Connections Only au Never Autoplay Videos.

Hatua hizo zinafanana pia kwa watumiaji wa Android, utakapofika kwenye Settings chagua Media and Contacts > Autoplay > On Wi-Fi Connection Only.

Kwa Instagram, fuata hatua zifuatazo ili kudhibiti kiwango cha matumizi ya data: Nenda kwenye Profile yako kisha fungua Settings. Washa kitufe cha Use Less Data chini ya Cellular Data Use, itakutahadharisha kuwa inaweza kuathiri jinsi utakavyotumia mtandao wa Instagram mfano kuchelewa kuona picha au video.

Kumbuka, jinsi ya kupata mipangilio hii inaweza kubadilika kutokana na jinsi muonekano wa programu tumishi za mitandao ya kijamii (app user interface) itakavyokuwa baada ya kusasishwa (update).

Kuangalia video na kusikiliza muziki mtandaoni
Mabadiliko ya teknolojia ya mawasiliano yametuongezea hitaji la kuangalia video mtandaoni, huku baadhi ya makampuni kama Netflix na Amazon yakituwekea maudhui yanayotushawishi kutumia gharama yoyote kuangalia kipenda roho.

Kwa wastani, unapoangalia video Netflix kwa kiwango cha 480p au 720p, unatumia kati ya MB 800 na GB 1.3 kwa saa, na pale utakapobadilisha ubora wa video kufikia 1080p, 1440p au 4K, kiwango cha matumizi ya data kinaongezeka kufikia GB 1.9 kwa saa au zaidi. Kwa Amazon, tegemea kutumia MB 800 kwa saa kwa kila video yenye kiwango kizuri unayoiangalia.

YouTube haina tofauti sana. Unaweza kutumia hadi MB 260 kwa saa kuangalia video yenye ubora wa 480p, wakati video yenye ubora wa kiwango cha juu (HD: 720p na 1080p) inaweza kukugharimu hadi GB 1.65 kwa saa. Video ya 4K huweza kutafuna hadi GB 2.7 za data kwa saa.

Si video tu, hata kiwango cha matumizi ya data kwa kusikiliza muziki mtandaoni kinatofautiana kutokana na kiwango cha ubora wa sauti utakachokichagua. Baadhi ya majukwaa ya muziki mtandaoni kama vile Apple Music na Spotify yanakupa uhuru wa kuchagua kiwango cha ubora, kama vile Low, Normal na High. Kwa kiwango cha Low, unaweza kutumia wastani wa MB 43 kwa saa, Normal inaweza kufika hadi MB 72 kwa saa na kwa kiwango cha High inaweza kufika MB 115 kwa saa.
Viwango vyote hivi ni makadirio ya wastani, na huweza kubadilika kutokana na kiwango cha ubora wa upatikanaji wa mtandao wa intaneti unaoutumia.

Njia rahisi ya kuangalia video au kusikiliza muziki mtandaoni bila kukunja nafsi kwa wasiwasi wa kuishiwa bando ni kupunguza kiwango cha ubora wa video au muziki. Ingawa unaweza kukosa ubora unaoutaka, utakuwa na uhakika wa kuendelea kutazama au kusikiliza kwa muda mrefu zaidi.

Unawezaje kufahamu kiwango cha data unachokitumia mtandaoni?
Pengine ungependa kufuatilia matumizi yako mtandaoni kwa sababu tofauti, ikiwamo kujiwekea ukomo wa kiwango cha matumizi. Teknolojia inakuruhusu kufanya hivyo.

Kwa watumiaji wa iPhone, nenda kwenye Settings > Mobile > Mobile Data Usage. Hapo utaweza kuona kiwango cha matumizi yako ya data. Na kwa watumiaji wa Android, fungua Settings kisha fungua Data Usage chini ya Network & Internet.

Download Now 782
Install Android App
Developer: Tanzania Tech Media
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot