NIGERIA: Mchungaji na Mkewe Mbaroni kwa Kushirikiana Kumbaka binti wa Miaka 16

1 year ago By Nyimbo Mpya 524
Are you a music lover looking for the latest track to add to your playlist? Look no further. Get ready for an unforgettable musical experience as we present a song by NIGERIA: Mchungaji na Mkewe Mbaroni kwa Kushirikiana Kumbaka binti wa Miaka 16.

NIGERIA: Mchungaji na Mkewe Mbaroni kwa Kushirikiana Kumbaka binti wa Miaka 16


JESHI la Polisi Jimbo la Ogun linasema kuwa limemkamata mchungaji mmoja kwa tuhuma za kula njama na mkewe kumbaka msichana wa miaka 16.

Taarifa kutoka kwa kikosi hicho cha polisi nchini Nigeria ilisema Mchungaji Peter Taiwo alikamatwa tangu Ijumaa ya wiki iliyopita katika Kanisa la Christ Apostolic Bible Church huko Alaja Oke, Abeokuta.

Polisi wanasema mkewe, Elizabeth, pia alikamatwa kwa tuhuma za kula njama ya ubakaji. Aidha, polisi wanasema waliwakamata watuhumiwa hao baada ya msichana huyo kuwalalamikia kuhusu tukio hilo.

Msichana huyo alieleza kuwa alipokwenda kanisani katika mazoezi ya kwaya, mke wa mchungaji alimpigia simu na kumwambia aende kwenye chumba ambacho mchungaji huyo alikuwa akimtafuta kwani atampeleka. Aliingia chumbani na mchungaji akafunga mlango na kutumia nguvu kukidhi mahitaji yake.

Alieleza kuwa baada ya mchungaji huyo kumaliza alichokuwa akifanya, mkewe aliingia chumbani humo na kumkuta akilia na kumsihi aache kulia na kumwambia kuwa sasa yeye ni mwanamke huku akimwonya kuwa asithubutu kusema yaliyotokea.

Aliambiwa kuwa iwapo atamwambia mtu yeyote basi atakufa. Polisi wanasema bado wanaendelea na uchunguzi na watawafikisha washukiwa hao mahakamani. Hata hivyo washukiwa hao tayari wamekiri mashtaka hayo ya ubakaji.

Chanzo: Global Publishers

Download Now 524
Install Android App
Developer: Tanzania Tech Media
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot