Mzee wa Upako asema haya kuhusu chanjo ya Covid-19

2 years ago By Mzee wa Upako asema haya kuhusu chanjo ya Covid 804
Are you a music lover looking for the latest track to add to your playlist? Look no further. Get ready for an unforgettable musical experience as we present a song by Mzee wa Upako asema haya kuhusu chanjo ya Covid9.

Mzee wa Upako asema haya kuhusu chanjo ya Covid19


Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’ ametoa wito kwa Watanzania kuwa na imani na Serikali kuhusiana na utoaji chanjo ya ugonjwa wa corona.

Mzee wa Upako ametoa rai hiyo leo Jumatano Julai, 28, 2021 katika hafla ya uzinduzi wa chanjo ya covid–19 iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

Amesema ili kupambana na janga hilo lililokumba ulimwengu mzima ni lazima nchi iwe na umoja na kushirikiana kwa pamoja kwani Serikali imejiridhisha vya kutosha juu ya chanjo hiyo.

“Wote tunakubali kwamba corona ni vita na hatuwezi kuishinda kama hatuna umoja, tuna Wizara ya Afya, Waziri Mkuu yupo sidhani kama hawa wenzetu wanaweza kuitoa nchi kafara kwamba watu wapate chanjo halafu wafe, lazima mifumo ya nchi yetu imejiridhisha, haitakuwa 100 kwa 100 kila kitu kina mapungufu lakini tujenge imani,”

“Mimi ni muhubiri wa zamani nilianza kuhubiri injili wakati wa Kambarage niwaombe maaskofu wenzangu tujenge imani kwa Serikali yetu na Wizara ya Afya, tunachanja kwa nia njema kwa ajili ya afya zetu, watakaosema Mzee wa Upako anajipendekeza sawa tu kwani akutukanaye hakuchagulii tusi,” amesema.

Ameongeza kuwa watu walimnukuu vibaya Hayati Dk John Magufuli kwani hakusema watu wasichukue chanjo bali umakini uwepo na kwamba tayari wameshajiridhisha kuwa nchi itakuwa salama.

“Uzuri Tanzania ni nchi ya ajabu katika Bara la Afrika hivyo tusiogope wala kufadhaika kwani tunafanya haya kwa nia njema,” amesema Mzee wa Upako.

Chanzo: Mwananchi

Download Now 804
Install Android App
Developer: Tanzania Tech Media
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot