MSICHANA AONGOZA WEZI KUIBA EKARISTI KANISANI

1 year ago 673
Are you a music lover looking for the latest track to add to your playlist? Look no further. Get ready for an unforgettable musical experience as we present a song by MSICHANA AONGOZA WEZI KUIBA EKARISTI KANISANI.

MSICHANA AONGOZA WEZI KUIBA EKARISTI KANISANI


Na Mwandishi wetu,

VIJANA 12 wanaotuhumiwa kuwa ni wezi wamejeruhi watawa watatu wa Kanisa Katoliki mkoani Pwani na kuiba ekaristi takatifu na kikombe kiitwacho sivorium.

Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Don Bosco, Padri Benno Kikudo alisema jana kuwa katika tukio hilo lililojiri Vikuge, kata ya Kongowe wilayani Kibaha kwenye nyumba ya watawa, vijana hao walikuwa wakiongozwa na mwanamke. Alisema tukio hilo lilijiri Jumamosi saa 7:00 usiku baada ya vijana hao kuvamia nyumba ya watawa wa shirika la Betania kutoka India.

Alisema mmoja wa watawa hao alikatwa jichoni kwa kutumia kitu chenye ncha kali akatokwa na damu nyingi na kukimbizwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Tumbi. “Vijana hao walipofika kwenye nyumba hiyo ya watawa walivunja milango kwa kutumia tofali na kufanya uhalifu huo kisha wakatoweka kusikojulikana,” alisema
Padri Kikudo.

Alisema watuhumiwa hao baada ya kuingia ndani ya nyumba ya watawa, waliingia kwenye kanisa wanalosali watawa hao na kuchukua vitu vyenye thamani ikiwemo ekarist na kikombe.

Mganga Mkuu wa Hopitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani ya Tumbi, Edward Wayi alisema walipokea watawa watatu, wakiwa na majeraha. Alisema waliwafanyia uchunguzi, wakapata matibabu na kisha wakaruhusiwa ili waendelee kutibiwa wakiwa kwenye makazi yao.

Chanzo: Habari Leo

Download Now 673