Morgan Heritage watangaza Collabo mpya na Diamond Platnumz — citiMuzik
Kundi hatari kabisa la muziki kutoka nchi ya Jamaica, Morgan Heritage wametangaza kutoa collabo nyingine mpya na msanii nguli wa Bongo Fleva kutoka katika lebo ya WCB Wasafi, Diamond Platnumz.
Kupitia ukurusa wao instagram , wameeleza mashibiki wake kuwa tayari kwa collabo kali kutoka kwao mwaka huu 2022.
“Mko tayari kwa collabo ingine na kaka yetu @diamondplatnumz? @gotmojomorgan anapoungana na Simba unajua tuko na kitu kali,” Heritage Morgan ilisema
Kundi la Morgan Heritage lina wasanii watano ambao ni watoto wa msanii Denroy Morgan ambaye alihamia Marekani kufanikisha safari ya muziki.
Ikumbukwe si mara yao ya kwanza kufanya Collabo na Diamond ambapo wamefanya collabo ambayo mwaka huo iliibuika kuwa miongoni mwa nyimbo zilizotamba sana.