Mh. Kassim Majaliwa: Serikali Itaendelea Kusimamia Uhuru wa Kuabudu

2 years ago By Nyimbo Mpya 814
Are you a music lover looking for the latest track to add to your playlist? Look no further. Get ready for an unforgettable musical experience as we present a song by Mh. Kassim Majaliwa: Serikali Itaendelea Kusimamia Uhuru wa Kuabudu.

Mh. Kassim Majaliwa: Serikali Itaendelea Kusimamia Uhuru wa Kuabudu


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kusimamia uhuru wa kuabudu kwa kila mwananchi kwa mujibu wa Katiba.

Alisema kuwa Serikali itaendelea kuheshimu uhuru huo wa ibada zinazoendeshwa katika nyumba za dini na itaendelea kushirikiana na taasisi zote za dini na madhehebu yote kwa ajili ya ustawi wa taifa na watu wake.

“Pale mtakapo pata tatizo lolote linalohitaji kutatuliwa na Serikali
waoneni viongozi wa Serikali walioko katika maeneo yenu, maelekezo ya serikali ni lazima viongozi hao waunge mkono jitihada za dini katika kufanya taifa hili kuwa tulivu.”

Akizungumza na waumini wa kanisa hilo, Waziri Mkuu amesema ni muhimu Watanzania kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kujiongezea kipato, kujiletea maendeleo ya mtu mmoja moja na Taifa kwa ujumla.

Aidha alisema kuwa, Kwa sasa Nchi ya Tanzania iko katika uchumi wa kati na mafanikio hayo yametokana na kujitoa na kuchapa kazi kwa Watanzania na kuwataka kuendelea kudumisha amani na kuiunga mkono Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

“Nitoe rai kwa Watanzania kutokubwetekana na mafanikio yanayopatikana Nchini, endeleeni kufanya kazi kwa bidii katika sekta zote na malengo yetu ni kila Mtanzania ajipatie kipato halali, kulipa kodi na kuchangia ukuaji wa uchumi wa Nchi yetu.”

Hata hivyo ametoa rai kwa Watanzania wanaoishi katika maeneo yanayoanza kupata mvua za vuli na masika kutumia vyema fursa ya msimu wa mvua hizo kujishughulisha katika kilimo ili kupata mavuno mengi zaidi.

“Mavuno mengi yatatuhakikishia usalama wa chakula na kutupatia ziada ya kuuza ndani na nje ya nchi yetu na kwakufanya hivyo tutakuwa tumetekeleza maagizo ya maandiko matakatifu na ya Serikali.

Waziri Mkuu alisema Serikali inatambua na kuunga mkono kamati za maendeleo ya kijamii zinazoundwa na viongozi wa dini na kuwasihi kutumia kamati hizo kuliombea Taifa na viongozi pamoja na kusimamia malezi ya vijana kuanzia ngazi ya familia kwa kutoa elimu ya kiroho.

hivyo kanisa limechangia mitungi ya oksijeni yenye thamani ya Shilingi Milioni mbili katika Hospitali ya Wilaya ya Nzega kwa ajili ya wagonjwa wenye changamoto ya upumuaji.

Chanzo: IPP

Download Now 814
Install Android App
Developer: Tanzania Tech Media
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot