Mchungaji wa Nigeria Asaidia Wasio na Makazi, Chakula Texas

2 years ago By Nyimbo Mpya 659
Are you a music lover looking for the latest track to add to your playlist? Look no further. Get ready for an unforgettable musical experience as we present a song by Mchungaji wa Nigeria Asaidia Wasio na Makazi, Chakula Texas.

Mchungaji wa Nigeria Asaidia Wasio na Makazi, Chakula Texas


Mchungaji Shetigo Nakpodia wa Kanisa la Redeemer’s Praise Church nchini Marekani ameingia kwenye trending headlines kwa kusaidia watu wengi wenye ukosefu wa makazi na Chakula huko San Antonio, Texas.

Mchungaji huyo amekuwa akiishi nchini Marekani akitokea Nigeria tangu mwishoni mwa miaka ya 90, kufuatia wito wa Mungu juu ya maisha yake katika kuomba na kuwasaidia watu wenye uhitaji.

Huduma hii ilimuongoza kununua jengo la kihistoria ambalo sasa ni kanisa linalojulikana kama Redeemer’s Praise ambapo yeye na timu yake wanahudumia watu 300 kwa kuwapatia chakula kila Jumamosi.

“Bwana aliweka mzigo moyoni mwangu kuendelea tu kuwasaidia hivyo na kuwalisha, Japo hofu ipo kuhusu Corona lakini najua Mungu atanilinda, Ikiwa COVID haitawaua, njaa itawaua” alisema Mchungaji Shetigo Nakpodia wa Kanisa la Redeemer’s Praise Church.

Karibu watu 3,000 huko San Antonio wanauhitaji mkubwa wa makazi, chakula, na maji kila siku. Mamlaka ya eneo hilo zinaripoti ongezeko la asilimia 2 tangu mwaka jana, wakisema asilimia 50 ya watu wa eneo hilo hawana akiba yoyote.

Mchungaji huyo kwasasa anaendesha kampeni ya kukarabati kanisa hilo katika kile anachokiita “Love Community Center,” ambapo wasio na makazi wanaweza kusafisha nguo zao na kupata chakula kizuri. Pia ana hamu ya kusaidia watu hao wasio na makazi kupata elimu ya diploma (general education diploma).

“Kwa hiyo Kila siku wapende watu, nenda kafanye kazi, tunza familia yako. Usiache kumwamini Mungu, pamoja na imani yetu tutashinda,” Nakpodia alisema.

Chanzo: CBN

Download Now 659
Install Android App
Developer: Tanzania Tech Media
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot