Mchungaji Kortini Kwa Kuuza Mafuta Anayodai Yanatibu Covid19
Askofu Climate Wiseman mwenye asili ya Kenya amefikishwa mahakamani huko nchini uingereza kwa tuhuma za kuuza mafuta anayodai yanatibu COVID19.
Askofu huyo anayeishi Uingereza anakabiliwa na Mashtaka ya udanganyifu na kufanya Biashara isiyo na usawa (fairness).
Hakimu wa Mahakama ya Lavender Hill ameshindwa kutoa hukumu kwakuwa suala hilo ni Uhuru wa Dini na kuabudu. Kesi imehamishiwa Mahakama nyingine na itasomwa Septemba 13.
Askofu Wiseman amekuwa akichunguzwa tangu Aprili mwaka jana kwa kutangaza tiba kupitia mafuta hayo kwa waumini wa kanisa lake. Chupa ya mafuta hayo iliyowekwa chapa ya Plague Protection Divine Oil, ilikuwa ikiuzwa karibu Euro 91 (Shilingi 247,000 za Kitanzania).
Ripoti zilionyesha kuwa mafuta hayo yametengenezwa kutokana na mchanganyiko wa mti wa cedar wood na hyssop ,mimea ya bustani jamii ya mint.
Chanzo: Nation Africa