Mchungaji Adai Malipo Zaidi Baada ya Kumponya Muumini

2 years ago By Nyimbo Mpya 808
Are you a music lover looking for the latest track to add to your playlist? Look no further. Get ready for an unforgettable musical experience as we present a song by Mchungaji Adai Malipo Zaidi Baada ya Kumponya Muumini.

Mchungaji Adai Malipo Zaidi Baada ya Kumponya Muumini


Mchungaji kutoka eneo la Maua, kaunti ya Meru nchini Kenya alikipata cha moto baada ya kutaka apewe sadaka nyingi zaidi kwa kazi aliyoifanya kwa jamaa aliyekuwa amemuombea akapona.

Inasemekana kuwa Pasta alisifika sana kwa kuombea wagonjwa wengi waliopona kando na kufanya miujiza mbali mbali kanisani vijijini. Kwa mujibu wa mtandao wa Taifa Leo, Jamaa alikuwa kitandani kwa zaidi ya mwaka mmoja akiugua maradhi ambayo hayakutambulika na wauguzi.

Baada ya familia kupata Habari za mchungaji huyo ndipo walifika kanisani kumuomba mchungaji aende kumuombea jamaa yao. Taarifa zinasema kwamba mtumishi huyo alifunga safari na kufika kwa jamaa huyo aliyekuwa amepoteza matumaini.

Baada ya maombi ya pasta jamaa alianza kupata nafuu siku baada ya nyingine hadi akapona kabisa ndani ya kipindi cha wiki mbili. Inaarifiwa kwamba jamaa na familia yake walianza kujiandaa kukutana na pasta kutoa shukrani zao ila wakashangaa pasta alipowabishia na kudai wampe sadaka nono kwa kuokolewa kwa mpendwa wao.

“Mbona hamkunitafuta kwa bidii punde tu jamaa yenu alipopona kama mlivyonitafuta alipokuwa mgonjwa? mnasikia sifa za uponyaji wangu Kijiji kizima ila nashangaa bado mmelaza damu badala la kuchangamka kuleta shukrani,” pasta alijitamba.

Inaarifiwa kwamba matamshi yaliudhi familia ya jamaa huyo haswa pasta alipokosa subira na kuwapuuza walipomueleza kwamba walikuwa wakijipanga ili wamtembelee. Baada ya mabishano ya meneno pasta huyo aliwasusa na wakaamua kuondoka bila kumpa chochote.

Walioshuhudia kisa hicho walisema kuwa pasta aliondoka kwa machungu huku akirushia familia hiyo mkono kama ishara ya kuwalaani kwa kumfukuza.

Taarifa zinasema baadhi ya wafuasi wa pasta huyo walidai familia ilikosea kwa kumfukuza lakini pia pasta alikosa hekima kwa kuishinikiza apewe kitita cha pesa.

Chanzo: TUKO

Download Now 808
Install Android App
Developer: Tanzania Tech Media
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot