Mcheza Mieleka Maarufu “The Undertaker” Azungumzia Safari Yake Ya Kiroho

1 year ago 789
Mcheza Mieleka Maarufu “The Undertaker” Azungumzia Safari Yake Ya Kiroho. Get ready for an unforgettable musical experience as we present new song by Mcheza Mieleka Maarufu “The Undertaker” Azungumzia Safari Yake Ya Kiroho Stream and download below.

Mcheza Mieleka Maarufu “The Undertaker” Azungumzia Safari Yake Ya Kiroho Song


Aliyekuwa mchezaji maarufu wa Mileka Duniani (WWE) Mark Calaway anayejulikana kama “Undertaker,” alifunguka juu ya safari yake ya kiroho kama Mkristo na kwa jinsi alivyojfunza kuishi maisha yake kulingana na kusudi la Mungu.

Katika mahojiano na Ed Young kwenye Mkutano mmoja wa Kikristo wa the C3 Christian Conference, Calaway alielezea kuwa alikulia katika familia ya Wakatoliki na aliamini katika Mungu, lakini mtindo wake wa maisha haukuonyesha kwenda sawa na Imani yake.

“Nimekuwa nikimwamini Mungu lakini sikuweza kuishi maisha yanayompendeza Mungu,” alisema. “Niliishi maisha mazuri kupita kiasi na sikuwa naishi maisha yangu kwa ajili ya Mungu.”

Calaway, ambaye hivi karibuni alitangaza kustaafu kwake kutoka kwenye mashindano ya mchezo wa mileka (WWE) ambapo alikuwa mtaalam mchezo huo wa mieleka kwa muda wa miaka 30. Kwa wakati huo aliweza kuchumbiana na mpambanaji mwenzake, Michelle McCool na hao wawili walikuja kuoana.

Alieleza kuwa Mkewe Michelle alikuwa akihudhuria ibada na mafundisho ya kiroho katika Kanisa la Lake Hills huko Austin, Texas Marekani na siku moja akamwomba aambatane naye kanisani hapo na huo ukawa ndipo mwanzo wa maisha yake ya Kiroho kuanza kubadilika.

Download Now 789