Matokeo 8 ya Kukosa Muda wa Kujifunza Neno la Mungu

1 year ago 474
Matokeo 8 ya Kukosa Muda wa Kujifunza Neno la Mungu. Get ready for an unforgettable musical experience as we present new song by Matokeo 8 ya Kukosa Muda wa Kujifunza Neno la Mungu Stream and download below.

Matokeo 8 ya Kukosa Muda wa Kujifunza Neno la Mungu Song


Matokeo 8 ya Kukosa Muda wa Kujifunza Neno la Mungu

Na. Mwl. Nickson Mabena.

Roho Mtakatifu amenijulisha mambo yanayotokea kwa watu kukosa Muda wa KUJIFUNZA NENO LA MUNGU na KUKOSA MUDA WA KUOMBA;

Kwa kukosa KUTUMIA MUDA KUJIFUNZA NENO LA MUNGU na KUTUMIA MUDA KWENYE MAOMBI haijalishi kwa kisingizio kwamba watu wapo bize au hawapo bize, KUNA AINA ZA WATU WANAOZALIWA. Hapa Nataka nikutajie AINA NANE ZA WATU WANAOTOKANA NA KUKOSA MUDA WA KUJIFUNZA NENO LA MUNGU NA KUKAA KWENYE MAOMBI KWA MUDA MREFU!.

1. TUMEKUWA NA WATU WAONGEAJI MAMBO YA HOVYO!.

Kuongea sio shida, shida huja pale unapoongea hovyo. Nikiwa na maana kwamba unaongea pumba, huku ukipenda zaidi kuongea mambo ya watu tu kwa kifupi unakuwa mmbea.

Yesu alisema “KINYWA CHA MTU HUNENA YAUJAZAYO MOYO WAKE”

Kwenye moyo wako USIPOJAZA NENO LA MUNGU bila shaka kuna matakataka kibao utayajaza humo, hivyo utakuwa unayaongea hayo tu!.

•UKIKOSA muda wa kukaa kwenye MAOMBI KWA MUDA MREFU, Bila shaka utakuwa na MUDA wa kukaa kwenye Vijiwe vya umbea, kwenye vibanda umiza au kwenye tv kwa muda mrefu wakati huna hata muda wa KUKAA KWENYE MAOMBI.

Mtu ANAYETUMIA MUDA WAKE KWENYE MAOMBI NA KUJIFUNZA NENO LA MUNGU, MDOMO WAKE UNAKUWA NA ‘LIJAMU’ HAWEZI KUONGEA HOVYO HOVYO.

2. WATU WANAOENENDA KWA KUONA BADALA YA KUENENDA KWA IMANI

“(Maana twaenenda kwa imani, si kwa kuona.)” 2 Kor 5:7 SUV

Tumekuwa na watu WANAOENENDA KWA KUONA si KWA IMANI badala ya *KUENENDA KWA IMANI SI KWA KUONA.

Kwasababu gani?

Biblia inasema IMANI CHANZO CHAKE NI KUSIKIA na KUSIKIA HUJA KWA NENO LA KRISTO; Kwahiyo kama HUNA MUDA WA KUJIFUNZA NENO LA KRISTO HUWEZI KUENENDA KWA IMANI, na ILI ‘KUONA’ KUSIWE NA NAFASI IBAKI IMANI PEKE YALE UNAHITAJI KUWA NA MFUMO WA KUFANYA MAOMBI KWA MUDA MREFU!.

Ukienenda kwa kuona, ni rahisi kuwa na HOFU pia ni rahisi KUHARIBIKIWA kwasababu UTAKUWA UNATUMIA MWILI ZAIDI KUTAFSIRI MAMBO YA ROHO.

Kumbuka Biblia inasema PASIPO IMANI HAIWEZEKANI KUMPENDEZA MUNGU!.

3. TUMEKUWA NA WATU WAUFUATAO MWILI

Maandiko yapo wazi kabisa, KILA MTU AJUE KUUWEZA MWILI WAKE!

“kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima;” 1 The 4:4 SUV

Pia Biblia inasema “Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu.”
Rum 8:8 SUV

Kwahiyo UNATAKIWA KUJUA KUUWEZA MWILI WAKO ILI UWEZE KUMPENDEZA MUNGU, lakini Kwa maisha kama hayo ya KUPENDA KULA KULA, KUTOPENDA KUJIFUNZA NENO LA MUNGU NA KUTOPENDA KUOMBA HUWEZI KUWEZA KUUWEZA MWILI WAKO!

Mwili wako usipojua KUUWEZA utakukwamisha kwenye mambo mengi sana.

“kwa maana kama tukiishi kwa kufuata mambo ya mwili, mwataka kufa; bali kama mkiyafisha matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi.” Rum 8:13 SUV

4.TUNA WATU WANAOWAZA KAMA DUNIA INAVYOWAZA

Kuna namna DUNIA inawaza KINYUME KABISA NA NENO LA MUNGU

Inasikitisha sana kuona na KANISA LINAWAZA KAMA DUNIA.

Biblia inasema WALA MSIIFATISHE NAMNA YA DUNIA HII;

“Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.” Rum 12:2 SUV

Ili UGEUZWE NIA (MIND) (UWAZE TOFAUTI NA DUNIA INAVYOWAZA) , UNAHITAJI MAFUNDISHO SAHIHI YA NENO LA MUNGU PAMOJA NA KUOMBA ILI MAFUNDISHO HAYO YAZAE MATUNDA KWENYE MAISHA YAKO!.

Kuifatisha namna ya Dunia ni KUWAZA KAMA DUNIA INAVYOWAZA!.

Watu wengi ambao wanayapinga sana mambo ya KIROHO ni WALE AMBAO HUWA HAWANA MUDA KABISA WA KUJIFUNZA NENO LA MUNGU na WASIO NA MUDA WA KUOMBA KWA MUDA MREFU!.

5. TUNA WATU WENYE MAZOEA

-Watu wanaoenda Kanisani kimazoea
-Watu wanaotumika kimazoea
-Watu WASIO NA BADILIKO LOLOTE
-Watu waliodumaa sana kiroho
-Watu wasiokua na kuendelea!
-Watu wasio na MAHUSIANO BINAFSI NA MUNGU!.

6.TUNA WATU WANAOTESWA NA DHAMBI ZA WAZI NA DHAMBI ZA SIRINI

-Tuna watu wanaoteswa sana na DHAMBI, Wengine wamehangaika sana kutafuta suluhu bila shida. TATIZO NI KUKOSA MAFUNDISHO SAHIHI YA NENO LA MUNGU.

Tuna vijana wanaotazama picha na video za ngono, wanaojichua, mashoga na makahaba huku wapo Kanisani.

(HAPA NISIWEKE MAELEZO MENGI, KAMA UNAHITAJI KUSAIDIWA KIROHO AU UNAHITAJI KUSAIDIWA KUJINASUA KWENYE MAISHA YA DHAMBI, NITAFUTE ILI NIKUSAIDIE KWA UPENDO)

7. TUNA WATU WANAOTESWA NA NGUVU ZA GIZA PAMOJA NA MAGONJWA YA MWILI

Kuna siku niliwahi kusema “KANISA LISILOOMBA, NI MAKAO YA DHAMBI, MAPEPO NA MAGONJWA”

Asikudanganye mtu, UNA AFYA MGOGORO KWASABABU YA KUKOSA MAARIFA SAHIHI YA NENO LA MUNGU na KUKOSA KUWA NA MAISHA YA MAOMBI!

Magonjwa yamekuwa yanakuonea sana, SULUHU IPO KWENYE NENO LA MUNGU kwa bahati mbaya HUNA MUDA WA KUJIFUNZA, suluhu ipo kwenye MAISHA YA MAOMBI kwa bahati mbaya hauna hata muda wa KUOMBA,

-Unatembea na madawa kwenye mikoba unafikiri ni suala la kawaida, ni vile tu HUJAWA NA MUDA NA MUNGU!.

8. TUNA WATU WENYE MIZAHA SANA

“Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha*. Bali *sheria ya BWANA ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku.” Zab 1:1 – 2 SUV

-Heri WASIOKETI BARAZANI PA WENYE MIZAHA, BALI HUTUMIA MUDA WAO KUTAFAKARI SHERIA ZA BWANA MCHANA NA USIKU!.

UKIBADILISHA MFUMO WA MAISHA, UKAWA NA MUDA WA KUTOSHA WA KUJIFUNZA NENO LA MUNGU NA UKAWA NA MUDA WA KUOMBA NINAKUHAKIKISHIA MAISHA YAKO YATABADILISHWA KABISA!.

JE! UNA MUDA WA KUJIFUNZA NENO LA MUNGU NA KUOMBA KWA MUDA MREFU? FANYA TATHIMINI YA MAISHA YAKO KUPITIA SOMO HILI.

Download Now 474