Makanisa Bukoba yatakiwa kuzingatia taratibu za Corona

1 month ago 112
Makanisa Bukoba yatakiwa kuzingatia taratibu za Corona, download nyimbo mpya. Download hapa Makanisa Bukoba yatakiwa kuzingatia taratibu za Corona.

Makanisa mbalimbali katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera yametakiwa kuzingatia taratibu za afya zinazotolewa na wataalamu zitakazo saidia kujikinga na magonjwa ikiwemo corona.

Wito huo umetolewa na juzi mjini humo na Askofu wa Kanisa la Hema ya Ukombozi, King James, wakati alipokutana na Waandishi wa Habari.

Hata hivyo, Askofu huyo amesema kuwa katika Kanisa la Hema ya Ukombozi wameendelea na hatua za kujikinga na mlipuko wa corona kwa kuepusha mikusanyiko ya muda mrefu na kunawa mikono.

“Niseme tu watu tujenge tabia ya kuwa wasafi muda wote kwa kuoga na kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni.

“Sisi kanisani tumeweka mifumo ya madiaba yanayotiririsha maji pamoja na kufanya ibaada zetu kwa muda mfupi ili watu wawe salama,” amesema Askofu James.

Askofu huyo ameongeza kuwa kabla ya mlipuko huo walikuwa wanafanya ibada zetu kwa masaa saba lakini sasa wamepunguza kutoka masaa sita hadi matatu.

Emiriana Kamugisha ambaye anaishi jirani na kanisa hilo amesema kuwa kutokana na kanisa hilo kuwa na waumini wengi ingekuwa changamoto kama wao wenyewe wangekuwa hawachukui tahadhari.

“Naona wanazingatia usafi kunawa mikono pamoja na kuvaa barakoa hilo limekuwa likinipa imani kuwa wako salama…. hata uvaaji wa barakoa unazingatiwa vizuri kwa kila muumini,” amesema Emiriana.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Charles Mbuge Julai 23, mwaka huu akitoa tamko la Serikali kwa wananchi juu ya kutokuwa na mikusanyiko isiyo ya lazima, alisema endapo kuna umuhimu wa kuwapo na shughuli za kijamii lazima lazima ionbewe kibali. Alitaja maeneo ya misiba, yanaweza kuwa na mikusanyiko na kushindwa kujikinga.

Chanzo: Mtanzania

Download Now