Makanisa 10 yachomwa moto nchini Canada

2 years ago By Nyimbo Mpya 514
Are you a music lover looking for the latest track to add to your playlist? Look no further. Get ready for an unforgettable musical experience as we present a song by Makanisa 10 yachomwa moto nchini Canada.

Makanisa 10 yachomwa moto nchini Canada


Makanisa 10 yamechomwa huko Alberta, Canada, katika mashambulizi ambayo polisi wamehusisha tukio hilo na dhulma za kihistoria dhidi ya wenyeji.

Wachunguzi katika eneo hilo wamesema kuwa rangi za chungwa na nyekundu zilipakwa katika makanisa ya mji wa Calgary.

Kiongozi wa eneo la Alberta amesema mashambulizi hayo ni yenye “kuchukiza”.

Na yanawadia baada ya kubainika kwa makaburi ambayo hayakuwa yametambuliwa karibu na kanisa la zamani kwenye makazi ya shule ambako watoto wa wenyeji wakati fulani walilazimshwa kuhudhuria.

Ugunduzi huo umesababisha baadhi kutoa wito wa kufutwa kwa sherehe ya kitaifa kwa heshima ya siku ya Canada inayofanyika Julai 1.

Kiongozi wa eneo la Alberta Jason Kenney, Alhamisi, amesema kuwa moja ya maeneo yaliyochomwa ilikuwa ni Kanisa la ‘African Evangelical Church’ mji wa Calgary.

Alisema kuwa wafuasi wa kanisa hilo kwa kiasi kikubwa walikuwa ni waliokuwa wakimbizi waliotoroka nchi ambazo mara nyingi makanisa huchomwa au kuharibiwa.

“Hawa walikuja Canada wakiwa na matumaini kwamba wanaweza kuendeleza imani zao kwa amani,” aliandika katika ukurasa wake wa Twitter Bwana Kenney, ambaye ni wa msimamo mkali. “Baadhi yao wamefadhaishwa na mashambulizi kama hayo.

“Na hicho ndio chanzo cha chuki kwa kuzingatia dhulma za kihistoria zilipotufikisha. Tutafute umoja, kuheshimiana na maridhiano.”

Polisi huko Calgary imesema kuwa matukio hayo yalitokea kati ya Jumatano usiku na Alhamisi asubuhi na kwamba “maeneo yaliyoharibiwa yote ni sehemu za waumini wa Kikiristo”.

Moja ya eneo la kuabudu lilikuwa na mjane na liliharibiwa ili wavamizi waweze kupaka rangi ndani, amesema.

Taarifa kutoka kwa polisi imesema kuwa rangi hizo zilipakwa kwa mikono na kujumuisha nambari “215”, ambapo wachunguzi wanahusisha kitendo hicho na “sehemu mbaya zaidi ya kihistoria” – mfumo wa makazi ya shule wa Canada.

Serikali ilifadhili shule ambazo zilikuwa zinaendeshwa na makundi la kidini karne ya 19 na 20 lengo likiwa ni kujumuisha vijana wenyeji.

Mnamo mwezi Mei, mabaki ya watoto wenyeji 215 – wanafunzi wa shule kubwa huko Canada – yalibainika katika makaburi ambayo hayakuwa yametambuliwa eneo la British Columbia.

Makanisa kadhaa ya Kikatoliki yalichomwa mwezi uliopita eneo la magharibi katika jamii za wenyeji.

Polisi ilisema kuwa imejitolea kutekeleza kazi yake na kuhakikisha kuna kuwepo na maridhiano.

Lakini pia taarifa hiyo ilisema kuwa: “Uharibifu wa namna hiyo sio tu kwamba ni kinyume cha sheria – lakini pia kuna sababisha mgawanyiko zaidi, hofu na uharibu wa mji wetu.”

Chanzo: BBC

Download Now 514
Install Android App
Developer: Tanzania Tech Media
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot