Killy - The Greenlight EP DOWNLOAD — citiMuzik

4 months ago 562
Killy - The Greenlight EP DOWNLOAD — citiMuzik, download Nyimbo Mpya. Stream and Download Killy - The Greenlight EP DOWNLOAD — citiMuzik on Nyimbo Mpya.

Mwanamuziki kutokea himaya ya Konde Music Worldwide Killy kwa mara nyingine amechangamsha kiwanda cha Bongo Fleva baada ya kutangaza kuachia EP yake ya kwanza tangu aanze muziki aliyoipa jina la ‘The Greenlight’.

RELATED: Killy Ft Harmonize – Ni wewe (Prod. Hunter)

Killy ambaye kwa sasa anatikisa Afrika Mashariki na video ya ngoma yake ya ‘Ni Wewe’ alitangaza ujio wa mradi huo kupitia akaunti yake ya Instagram ambapo aliwashukuru watu wote walioshiriki kuandaa EP hiyo iliyosheheni ngoma tano.

Wasanii ambao wameshirikishwa kwenye EP hiyo ni Ibraah aliyeshiriki kwenye ‘Kiuno’ na Christian Bella ambaye ameshiriki kwenye ngoma ya ‘Niambie’.

Ngoma nyingine zote kama Vumilia’, ‘Itafika’ pamoja na ‘Ilete’ Killy amefanya peke yake.

Aidha, Killy pia aliwashukuru watayarishaji wa muziki watatu ambao ni Mocco Genius, Wambaga pamoja na Terriyo Monster kwa kuweza kushiriki kikamilifu kwenye EP hiyo ambayo alitanabaisha ametumia muda mwingi sana kuiandaa.

“Shukrani nyingi pia ziwaendee maproducer tulioshirikiana kutengeneza hizi nyimbo Terriyo Monster, Mocco Genius, Wambaga na wasanii wenzangu nilioshirikiana nao kukamilisha ep yangu ya kwanza kabisa The Greenlight EP. Pamoja na management yangu nzima ya Konde Gang bila kumsahau boss wangu Harmonize,” aliandika Killy.

RELATED: Harmonize – Teacher (Prod. Steve Spesho)

Killy anatarajiwa kuwa msanii wa pili kutokea Konde Gang kuachia EP yake tangu kuanzishwa kwa lebo hiyo, msanii wa kwanza akiwa ni Ibraah alipoachia EP yake ya ‘Steps’ mwaka 2020 na EP ya pili ya kuitwa ‘Karata Tatu’ aliiachia Januari mwaka 2021.

Killy – The Greenlight EP DOWNLOAD
Killy – The Greenlight EP DOWNLOAD

Also, check more tracks from Harmonize;

HTML tutorial
Download Now 562