Kenya: Wezi Wavunja Kanisa na Kuiba Nguo za Ndani za Pasta

1 year ago 330
Kenya: Wezi Wavunja Kanisa na Kuiba Nguo za Ndani za Pasta. Get ready for an unforgettable musical experience as we present new song by Kenya: Wezi Wavunja Kanisa na Kuiba Nguo za Ndani za Pasta Stream and download below.

Kenya: Wezi Wavunja Kanisa na Kuiba Nguo za Ndani za Pasta Song


Waumini wa Kanisa la Makutano PAG eneo la Lurambi, Kakamega, wanahesabu hasara baada ya wezi kuvunja kanisa hilo na kuiba mali yenye thamani isiyojulikana.

Wezi hao wanaripotiwa kuvunja kanisa la Makutano PAG na kuiba mali yenye thamani.Picha:UGC. Source: Facebook

Duru ziliarifu kwamba wezi hao waliiba mali kadhaa ikiwemo nguo za ndani za pasta na chakula chake jikoni. “Wezi hata wanaiba nguo za ndani za pasta wanaenda kuuza, hii ni nini?” alisema mmoja wa waumini Wycliffe Sajida, ambaye ndiye pasta wa kanisa hilo, alisema alipoteza kila kitu wakati wa kisa hicho. “Walichukuwa suti mbili, mashati matano, viatu, mtungi wa gesi, nguo za kuubiri na KSh. 2,500,” pasta Wycliffe alisema. Waumini wa kanisa hilo sasa wanataka idara ya polisi eneo hilo kuchukuwa hatua na kuwasaka wezi hao.

Katika tukio sawia na hilo lililoshuhudia Shinyalu, kaunti ya Kakamega, wanaume wawili wanaodaiwa kuiba nguruwe wa ajuza mmoja walianguka na kupoteza fahamu. Kulingana na ripoti ya polisi kwenye kitabu cha matukio (OB), mwanamke huyo ambaye alionekana mwenye masikitiko makubwa alitafuta huduma za mganga mmoja Kaunti ya Bungoma ambaye alimtembelea nyumbani kwake na kufanya ibada zake kabla ya kuondoka. “Karibu saa 1900, wanaume hao wawili walianguka. Mfuasi huyo alikuwa ameacha maagizo kwamba mtu yeyote atakayeathiriwa asichukuliwe hospitalini bali aachwe katika hali yoyote aliyokuwa nayo hadi asubuhi atakaporudi. Ndugu zao walisisitiza kwamba maagizo ya mfuasi wa ibada yazingatiwe. Ripoti ya maendeleo ya kesi ya PUI ifuatwe,” ilisoma ripoti ya polisi.

Je, unayo taarifa ya Kanisa/Kikristo ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia gospomedia@gmail.com au WhatsaApp: +25571065200

Chanzo: Tuko Kenya

Download Now 330