Kenya: Picha ya Raila Odinga Akisoma Biblia Kanisani Yazua Gumzo Mitandaoni

2 years ago By Nyimbo Mpya 660
Are you a music lover looking for the latest track to add to your playlist? Look no further. Get ready for an unforgettable musical experience as we present a song by Kenya: Picha ya Raila Odinga Akisoma Biblia Kanisani Yazua Gumzo Mitandaoni.

Kenya: Picha ya Raila Odinga Akisoma Biblia Kanisani Yazua Gumzo Mitandaoni


Kiongozi wa cha ODM Raila Odinga Jumapili Septemba alihudhuria ibada ya kanisa katika eneo la Butere ambapo askofu Rose Okeno alitawazwa mkuu wa dayosisi hiyo.

Picha ya Raila akiwa kwenye mimbari akisoma Biblia hata ilienea mtandaoni alipoipakia katika ukurasa wake wa Facebook. Wandani wake walisema ni ishara kuwa Raila anamwamini Mungu kinyume na madai ya wakosaoji wake ambao wamekuwa wakisema ni mtu anayeamini abracadabra.

Naibu Rais William Ruto ndiye humshambulia Raila sana akimuita ‘mganga’ kama njia ya kushuku imani yake kidini. “Ruto amekuwa akimuita Raila mganga, ni vizuri ajue kuwa Raila si mganga mbali ni mchungaji wa Bwana,” mwanamitandao Marigiri aliandika.

Neno ‘mganga’ huwa halikosi mdomoni mwa DP kila anapomshambulia Raila akimtaja kama mwanasiasa asiyependa kanisa. Raila Februari 9, akiongea Homa Bay wakati wa hafla ya kumuweka wakfu Askofu Michael Odiwa, alimtaka DP kukoma kumuita hivyo. “Mimi ni Mkristu wale ambao hunitaka kama mtu wa vitendawili na mganga wakome. Mganga ni mtu ambaye anatibu watu. Japo sina shida kuitwa hivyo, nataka kutambuliwa kama Mkristu wa kweli,” alisema

Ruto hujulikani kwa kuhudhuria kanisa ambapo amekuwa akishambuliwa kwa kutoa michango na harambee. Raila husema anatumia kanisa kwa njia isiyofaa ili kujitafutia umaarufu wa kisiasa kwenye safari ya kutafuta kura za kuingia Ikulu. Hata hivyo, yeye ameshikilia kuwa alilelewa kanisa na kujua maana ya kumtolea Mwenyezi Mungu mbegu.

Chanzo: TUKO

Download Now 660
Install Android App
Developer: Tanzania Tech Media
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot