Kenya: Pasta Atozwa Faini ya KSh2000 Baada ya Kufumaniwa na Mke wa Mtu

1 year ago 334
Kenya: Pasta Atozwa Faini ya KSh2000 Baada ya Kufumaniwa na Mke wa Mtu. Get ready for an unforgettable musical experience as we present new song by Kenya: Pasta Atozwa Faini ya KSh2000 Baada ya Kufumaniwa na Mke wa Mtu Stream and download below.

Kenya: Pasta Atozwa Faini ya KSh2000 Baada ya Kufumaniwa na Mke wa Mtu Song


Na Mwandishi Wetu,

Pasta wa Kanisa la African Divine eneo la Lugari, Kaunti ya Kakamega, ametozwa faini ya KSh2,000 baada ya kufumaniwa akifanya uzinzi na mke wa muumini wake.

Mhubiri huyo aliyetambuliwa kwa jina la Samuel pia alitozwa faini ya ng’ombe na kondoo kama adhabu kutoka kwa baraza la wazee wa jamii ya Kabras. Samuel alipatikana na hatia ya kufanya uzinzi na mke wa Charles Mulongo (Pichani) kwenye kitanda chao cha ndoa katika kijiji cha Mufutu siku ya Ijumaa, Mei 7 2021.

Kwa mujibu wa wazee hao, pesa hizo zitatumika katika kutakasa nyumba ya Mulongo ili kuzuia familia yake dhidi ya mapepo ya usherati. Wazee hao pia waliidhinisha talaka kati ya Mulongo na mkewe aliyekiri kuwa alifurahia uwezo wa mhubiri huyo kitandani baada ya mume wake kumtelekeza.

Mulongo alikuwa amemtembelea mke wake wa tatu ambapo alitarajia kulala usiku huo wa Alhamisi, Mei 7, Ndipo alipopokea taarifa kwamba majirani zake wamemkamata mtu wasiyemjua katika chumba chake cha kulala.

“Nilikuwa katika nyumba yangu nyingine wakati nilipopigiwa simu na mmoja wa majirani akinijulisha kuwa kuna mtu ameshikwa akiwa na mke wangu. Mwanamke hapaswi kukudharau kwa kiwango ambacho analeta wanaume chumbani kwako. Siwezi kuvumilia suala kama hilo,” alisema. Mulongo alisema kuwa ni kitendo ambacho hakukitarajia kwa kuwa alikuwa anaheshimu pasta Samuel ambaye amekuwa akitoa mahubiri moto moto kanisani. Tukio hilo linajiri wiki mbili baada ya Askofu mstaafu wa Kanisa la Kianglikana Uganda, Stanley Ntagali, kuomba msamaha hadharani kwa kushiriki mapenzi na mke wa mtu.

Mnamo Jumanne 27 Aprili 2021 mbele ya maaskofu wa Kianglikana na makuhani waliokusanyika katika Kanisa Kuu la Namirembe kusherehekea miaka 60 tangu kanisa hilo lianze kujitawala, Mchungaji huyo alikiri kuzini na Judith.

Chanzo: TUKO

Download Now 334