Kenya: Mganga Agombana na Pasta kwa Kujenga Kanisa Karibu na Makao Yake

2 years ago By Nyimbo Mpya 465
Are you a music lover looking for the latest track to add to your playlist? Look no further. Get ready for an unforgettable musical experience as we present a song by Kenya: Mganga Agombana na Pasta kwa Kujenga Kanisa Karibu na Makao Yake.

Kenya: Mganga Agombana na Pasta kwa Kujenga Kanisa Karibu na Makao Yake


Mganga mmoja kutoka eneo la Aloeti, Teso alisikika akiapa kumtimua mchungaji ambaye alianzisha kanisa karibu na boma lake.

Duru zinaarifu kwamba mganga alidai kwamba psta alikuwa na nia ya kumuangusha kibiashara kwa kumnyang’anya wateja wake.

Kwa mujibu wa Taifa Leo, mchungaji huyo anasemekana alikuwa amenunua kipande cha shamba kutoka kwa jamaa ambaye ni jirani wa mganga na kuanza kujenga kanisa. “Juzi nimesikika watu wakiomba hapa. Nani alikuambia hii sehemu inahitaji kanisa?” mganga alimuuliza pasta kwa ukali. Inasemekena kwamba mchungaji alianza kumnukulia mpoiga ramli vifungu vya Biblia. “Kaa na hiyo Biblia yako. Mimi nataka kujua aliyekuleta hapa na kukuambia ujenge kanisa karibu na boma langu,” mganga alizidi kuwaka.

Hata hivyo, pasta aliamua kumpuuza na kusonga mbele na shughuli yake mbali na alikokuwa mganga.

“Njama yako ninaijua. Fanya biashara zako na uniache pia mimi nifanye zangu,” mtumishi wa Mungu alisema. Kelele za mganga ziliwavutia majirani zake waliofika kwa haraka kujionea kilichokuwa kikiendelea. “Huyu jamaa sijui ametoka wapi. Hili kanisa walahi halitajengwa hapa,” mganga aliapa.

Penyenye zinasema pasta aliamua kukabiliana na mganga na kumuarifu kwamba lazima kanisa litaendelea kujengwa kama alivyopanga. “Hakuna kitu utafanya. Lazima hao wateja wako waje hapa kanisani waokoke. Hata wewe lazima utaokoka,” mchungaji alimfokea mpiga ramli.

Majirani walishindwa kustahimili vicheko kutokana na majibizano ya wawili hao. “Wewe hunijui vizuri. Hauwezi kujenga kanisa karibu na makao yangu. Nitalibomoa mimi mwenyewe. Lazima uiheshimu kazi yangu,” mganga aliapa. Semasema kutoka eneo hilo zilisema kwamba mpiga ramli huyo alikuwa amewapiga vita wahubiri wote wa kutoka eneo hilo, jambo lililofanya makanisa mengi kujengwa mbali na boma lake.

Hata hivyo, mchungaji alikaa ngumu akamwambia kuwa nguvu za giza haziwezi kushindana na Nuru.

Chanzo: TUKO

Download Now 465
Install Android App
Developer: Tanzania Tech Media
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot