Jeshi la Polisi latia Mguu Shule za Dini

2 years ago By Nyimbo Mpya 766
Are you a music lover looking for the latest track to add to your playlist? Look no further. Get ready for an unforgettable musical experience as we present a song by Jeshi la Polisi latia Mguu Shule za Dini.

Jeshi la Polisi latia Mguu Shule za Dini


Katika kile kinachoelezwa kuwa ni mkakati wa kukabiliana na uhalifu, yakiwamo matukio ya kigaidi, Jeshi la Polisi limepanga kuanza kuchunguza mitalaa ya mafunzo yanayotolewa katika vyuo na shule zote za dini.

Hatua hiyo inalenga kuhakikisha vyuo na shule zinazomilikiwa na taasisi za dini zinawafundisha watoto uzalendo na hakuna viashiria vya uvunjifu wa amani na matukio ya kigaidi. Mbali na vyuo na shule, uchunguzi huo utahusisha mafundisho ya madrasa na ‘Sunday School.’

Hayo yameelezwa juzi na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro, muda mfupi baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akitokea Rwanda, alikoenda kwa ziara ya siku tatu. Ziara hiyo ya IGP Sirro ililenga kuboresha ushirikiano wa matukio ya kihalifu.

IGP Sirro alisema hiyo ni hatua mojawapo ya kupambana na makosa ya kigaidi na yale yanayovuka mipaka kupitia kikosi maalumu cha kufuatilia mwenendo wa mafunzo katika nyumba za ibada iwapo yanajenga au yamelenga kuharibu nchi.

“Huu utaratibu wenzetu wa Rwanda wameufanya na tunaona ni mzuri, nasi tukiangalia namna ya kuuchukua, tutawashirikisha viongozi wa dini, wakiwamo maaskofu na masheikh. Timu yetu ya kupambana na makosa ya kigaidi itaangalia namna gani tupitie yale mafunzo yanayofundishwa kwenye Sunday Schools, madrasa, shule pamoja na vyuo vya dini kama yapo kwa ajili ya kuwajenga vijana wa Kitanzania au kuwabomoa. Ni uzoefu ambao tunauchukua na utatusaidia sana.

“Lingine kwa wale vijana ambao wameharibika walioingia kwenye mambo ya kigaidi wenzetu wamejenga majumba maalumu wanasema ni kwa ajili ya kufanya tiba maalumu za kuwarekebisha na sisi tutaona ni namna gani tutaongea na viongozi tukiwapata vijana wadogo tuone namna tutawarekebisha,” alisema IGP Sirro.

Vilevile, alisema wanaangalia namna gani watapambana na wahalifu wa makosa yanayovuka mipaka na kutoa tahadhari kwa wale wanaovunja sheria.

Alisema wamejipanga kupambana na wahalifu wa makosa yanayovuka mipaka, mfano usafirishaji haramu wa binadamu, matumizi na biashara ya dawa za kulevya pamoja na ugaidi na kwamba ameona jinsi Rwanda inavyokabiliana nayo.

Alitoa wito kwa Watanzania kutoa taarifa ikiwa kuna mtu wa karibu ambaye anaonyesha dalili za kujihusisha na vitendo hatari.

“Ukiona mtoto wako, ndugu yako au jirani anafanya jambo lisilo sahihi au ana dalili siyo nzuri tupeane taarifa.

“Kama una mke, mume, mjuukuu na unaona anabadilika na unahisi ni mhalifu au anashiriki makosa ya kigaidi ukatupa taarifa tukampata mapema tutakaa naye, sio lazima tumpeleke mahakamani, tutakaa naye tujue tumrekebishe ili arudi kuwa Mtanzania wa kawaida,” alisema Sirro.

Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Gervas Nyaisonga alisema Jeshi la Polisi ni watu wa usalama hivyo haoni kama suala hilo lina shida yoyote, ila akaangaliza kuwa ni vema wakashirikiana na mamlaka zilizotumika kusajili makanisa, misikiti, shule na vyuo vya kidini ili kuondoa mkanganyiko unaoweza kujitokeza.

“Wao ni wana usalama, kama kuna issue (jambo) linahusu usalama wa nchi ni kazi yao, shule zimesajiliwa na zinaendeshwa kwa mujibu wa sheria, lazima wafanye kazi na mamlaka husika ndiyo inayoelewa mitalaa, hiyo itasaidia kuondoa misuguano, wakifanya wenyewe watakosea.

“Sioni kizuizi, kwani jeshi linatimiza wajibu wao kiusalama, naamini wana sheria zao wanazozitekeleza na shule zinaendeshwa kwa mujibu wa sheria, kama kuna anayekiuka ni haki kuhakikisha usalama unakuwepo,” alisema Nyaisonga.

Katibu Mkuu wa Bakwata, Nuhu Mruma alisema baraza hilo halina shaka na hatua hiyo, lakini aliwataka watu watakaoutekeleza mchakato huo wawe na weledi kuhusu masuala ya dini.

“Tunamshauri IGP Sirro kama jambo hili lina nia nzuri na ili liende sawa kabla ya kutekeleza wakutane na viongozi wa dini na kushauriana namna ya kulifanya kuona njia sahihi na malengo yake. Lisipotafsiriwa vizuri hata hiyo timu yake haitafanya kazi kwa ufanisi,” alisema Mruma.

Mwalimu Mruma pia alisema mfumo wa dini ya Kiislamu unajitosheleza kwa kufuata vitabu na mafunzo na hawana shaka.

Alisema ana imani wanaofundisha dini kwa usahihi hawatakuwa na tatizo na ukaguzi utakaofanywa na polisi kwa sababu watakuwa safi.

“Kama kuna wengine wanatumia mwavuli wa dini kufanya mambo mengine, wakibainika au kugundulika ni sahihi wakichukuliwa hatua. Labda kuna jambo mahsusi wameliona sasa, kwa sababu hizi madrasa na vyuo vipo siku nyingi.

“Vinafundisha na hawa masheikh na viongozi wa dini tuliona nao wamefundishwa katika hizo madrasa. Kama kutakuwa na nyingine zenye malengo tofauti watazibaini kwa sababu wana ujuzi huo, kikubwa kinachotakiwa ni uangalifu na weledi katika mchakato huu,” alisema.

Wakili wa kujitegemea, Jebra Kambole alisema timu zinazoundwa na polisi kufuatilia jambo kuna baadhi zinashindwa kufanikiwa kwa sababu zinahusisha watendaji wa jeshi hilo peke yao ambao hukosa baadhi ya uzoefu.

“Ushauri wangu ni kuwepo kwa watendaji mchanganyiko ili timu ziwe huru, haki na usawa katika utekelezaji wa majukumu yaliyokusudiwa. Sidhani kama watafanikiwa katika mpango huo, kwa sababu sijajua ukomo wao utakuwa wapi,” alisema Wakili Kambole.

Chanzo: Mwananchi

Download Now 766
Install Android App
Developer: Tanzania Tech Media
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot