Ijue Nguvu unayopata Ukisoma Biblia

1 year ago 402
Ijue Nguvu unayopata Ukisoma Biblia. Get ready for an unforgettable musical experience as we present new song by Ijue Nguvu unayopata Ukisoma Biblia Stream and download below.

Ijue Nguvu unayopata Ukisoma Biblia Song


Wakristo wengi katika jamii ya waaminio wamepoteza nguvu ya kusoma Biblia, kwasababu hawana ufahamu kwamba Mungu ni Neno, hii pointi ni halisi kabisa hata Biblia imefunua katika Yohana 1:1-3.

Kutokana na Yohana 1:1 ukisoma Biblia maana yake unamsoma Mungu , vilevile moyo wako unafundishwa siri za ufalme wa Mungu.

Mkristo mwamini anaposoma Biblia maana yake moyo wake unahojiana na Mungu uso kwa uso, ndio maana Yesu Kristo alisema wazi katika Yohana 14:23.

Mkristo mwamini anayeiamini Biblia, akikaa chini kusikiliza Neno la Mungu yaani kufundishwa, akatoa muda wake kusoma Biblia mwamini huyu mpenyo ni lazima kwenye maisha yake yaani mafanikio ni lazima, kwasababu anakuwa ameyaishi mapenzi ya Mungu.

Mkristo anapotoa muda wake katika mambo makuu mawili
a). kujisomea Neno la Mungu mara kwa mara
b). kulisikiliza Neno la Mungu mara kwa mara katika Imani, maana yake anavalishwa asili moja na Mungu kwasababu mwamini akiliamini Neno la Mungu(Biblia) maana yake asili aliyonayo itafanana na asili ya Mungu, jambo hilli hata Biblia imelifunua kwa kina katika 1Wakorintho 6:17.

Mkristo mwamini huunganishwa na Neno la Mungu kupata Baraka zake anazozitamani kwenye uso wa Mungu.

Nguvu ya kusoma Biblia ndiyo itakayo nisaidia kuimarika katiaka ufahamu wa rohoni.
Nikijiona ninakosa hamu ya kusoma Biblia maana yake ninanyemelewa na kifo cha kiroho, kwa maana zaidi ninakuwa hai katika mwili, katika roho nimekufa. Jambo hili hata Ufunuo3:1 inasema.

FAIDA YA KUSOMA BIBLIA (KUSIKILIZA)
Kuna faida kuu mbili katika misha ya kristo anayetoa muda kusikiliza Neno la Mungu vilevile kujisomea Neno la Mungu.
A. Faida ya kwanza ni mkristo kupata ufahamu
B. Mkristo kupata mtiririko wa maombi

UFAFANUZI KUHUSU KIPENGELE “A” KINACHO ZUNGUMZIA UFAHAMU.
Maisha ya mkristo aliyeokoka yaani aliye mwamini Yesu kristo na kumkiri Yesu kristo kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake yanahitaji ufahamu zaidi wa rohoni, kwasababu wakristo waamini wanaishi, vilevile amezungukwa na jamii kubwa ya wasio amini, kwahiyo kabla ya jamii ya wasioamini hawajaanza kuiamini Biblia inatakiwa wanione mimi niliye okoka yaani ninaye iamini Biblia nikiyaishi maisha sambamba na kilicho andikwa kwenye Biblia kiusahihi.

Ufahamu ndio utakayo yafanya maisha ya mkristo aliyeokoka kuwa mvuto kwa jamii ya wasio amini.

Mkristo mwenye ufahamu huwa kuna mambo yanayo jitokeza kwenye maisha yake i. Hekima
ii. Upendo
iii. Utu
iv. Uvumilivu, Huyo anaweza kuitwa mkristo anayeishi sambamba na haki ya Mungu.

Ufahamu wa Neno la Mungu katika maisha ya mwamini ndio utakao yasaidia maisha ya mwamini kubadilika hapa inanipa picha haitakiwi nijitaabishe kwa mambo mengine bali katika kila jambo ni kushukuru, kwasababu katika pointi ya juu imenifunulia maisha ya mtu mwenye ufahamu ni vitu gani vinatawa katika maisha yake.

UFAFANUZI WA KIPENGELE “A” MTIRIRIKO WA MAOMBI
Hii inabidi ifahamike wazi na kwa kila asikiaye na aelewe, mtirirko wa maombi ataupata mtu kutokana na kina cha ufahamu wa Neno la Mungu katika moyo wake,na hii inanipa ufahamu zaidi maombi yenye imani au yanayoombwa na mtu mwenye imani yanatoka kwenye moyo wenye ufahamu wa ndani katika Neno.

Nikitaka kupata mtiririko wa maombi lazima niuhusu ufahamu wangu kupata utulivu wakati waa kusoma Biblia.

Maombi ya mkristo yanapata nguvu pale anaporuhusu Neno la Mungu kuyaongoza maombi hayo.

Ninapo litumia Neno la Mungu kwenye maombi yangu maana yake ninamtumia Roho Mtakatifu kuvunja ukuta alioniwekea shetani kati ya mimi na Baraka zangu.

Mahali ambapo kanisa linajengwa katika misingi ya kweli yaani ya Neno la Mungu kwa usahihi huwa kuna mambo kadha kujitokeza
i). Uponyaji
ii). Kutubu dhambi
iii). Kusamehewa dhambi
iv). Kufunguliwa
v). Kubarikiwa
vi). Madhihirisho ya nguvu za Roho Makatifu,Hayo ni mambo yatakayo onekana katika kanisa linalofundisha misingi ya kweli ya ucha Mungu.

Kibiblia maombi ya waamini yanatakiwa yasimamiwe au yaongozwe na Neno la Mungu,Hapo yatakuwa na mvuto wa kutetewa na Roho ambazo Mungu aziweka kwa lengo la kuleta Baraka kwetu,uponyaji,rehema, na mengineyo mengi na katika kitabu cha Waebrania Mungu kasisitiza Waebrania 1:14.

Download Now 402