Evelyn Joshua: Mfahamu mke wa muhubiri maarufu wa Nigeria TB Joshua

1 year ago 405
Are you a music lover looking for the latest track to add to your playlist? Look no further. Get ready for an unforgettable musical experience as we present a song by Evelyn Joshua: Mfahamu mke wa muhubiri maarufu wa Nigeria TB Joshua.

Evelyn Joshua: Mfahamu mke wa muhubiri maarufu wa Nigeria TB Joshua


Top Stories

Published on June 9, 2021

Nabii Evelyn Joshua aliyekuwa mke wa Temitope Balogun Joshua , ametuma ujumbe wake kwenye ukurasa wa Twitter akimuomboleza mume wake ulioonekana kuwatia moyo waomboleza, kufuatia kifo cha mumewe.

Amesema:”Kumpoteza mpendwa wako sio rahisi, iwe ghafla au kwa kifo kilichotarajiwa inaumiza kila mara. Kifo kinaweza kusambaratisha maisha yetu. Ndio maana ni muhimu kuwaendelea kuwa na Mungu. Yeye pekee ndiye anayeweza kupunguza maumivu yetu na kutufariji katika nyakati hizi. Kimbilia kwake”, uliandikwa ujumbe huo.

Losing a loved one is never easy; whether sudden or foreseen it’s always heartbreaking. Grief can wreak havoc on our overall well being. That’s why it’s important to stay rooted to the Almighty. Only He can lessen our heartache and comfort us in these times.
Seek refuge in Him. pic.twitter.com/HEpB8Ksgfr

— Mrs Evelyn™ Joshua (@Mama__Evelyn) June 6, 2021

Nabii Evelyn Joshua ni nani hasa?

Nabii Evelyn Joshua ni mke wa TB Joshua, Mhubiri wa televisheni tajiri na mwanzilishi wa kanisa la Synagogue, Church of All Nations.

Alizaliwa tarehe 17 Disemba 1968 katika eneo la Okala Okpumo, Jimbo la Delta nchini , Nigeria, kwa wazazi wake Bwana na Bibi Nicholas Akobundo.

Kwa hivyo basi mwezi Juni, 2021 Evelyn Joshua anatimiza umri wa miaka 52.

Evelyn Joshua alianza masomo yake katika Shule ya Msingi ya St Emecheta iliyopo katika mji wa Ezi, katika jimbo la Delta nchini Nigeria.

Mwaka 1977, alihamia katika mji wa Lagos na kuendelea na masomo yake katika shule ya msingi ya Orile na baadaye akaendelea na masomo ya sekondari.

Alipohitimu, alipata fursa ya kufanya kazi katika kampuni ya Nigerian Distilleries Ota, iliyopo katika jimbo la Ogun.

 Mfahamu mke wa muhubiri maarufu wa Nigeria TB Joshua

Ushawishi wake kwa kanisa

Evelyn Joshua amekuwa Muhimiri katika maisha ya mumewe na huduma yake ya kanisa.

Japo alionekana nadra sana kando ya mumewe wakati wa mahubiri ya mikusanyiko ya watu , Bi Evelyn ndiye Mkuu wa pili wa Kanisa la The Synagogue, Church of All Nations, na anasemekana amechangia pakubwa katika shughuli za huduma na maendeleo ya kanisa hilo.

Evelyn Joshua anaaminiwa kuwa ndiye mtu wa pili mwenye ushawishi zaidi katika kanisa la Synagogue baada ya mume wake.

Mara kwa mara amekuwa akikutana na kuwapa ushauri nasaha watu binafsi ambao hawakuweza kukutana na TB Joshua. Pia huhubiri kanisani.

Alivyokutana na Mume wake TB Joshua

Evelyne alikutana na Temitope Balogun Joshua wakati alipokuwa katika kazi zake na baadaye akawa mtu maarufu.

Manamo mwaka 1990, Evelyn alisafiri katika eneo la Egbe kumtembelea dada yake, wakati alipokuwa huko alikutana na mchungaji TB Joshua, ambaye alimzidi umri wa miaka miatano.

Alikuwa amekwenda kukutana naye kwa ajili ya kupata ushauri nasaha na muongozo wa kiroho , na mkutano wao ambao ulidumu kwa muda wa dakika arobaini na tano, ulikua chanzo cha safari yao ya ndoa.

Kulingana na marehemu nabii TB Joshua, kukutana na mke wake kulipangwa na ngumu, na alimuomba amuoe siku hiyo hiyo.

Evelyn alikuwa na hofu juu ya ombi la ndoa ambayo haijui, licha ya kwamba alisema ndio, na wakaoana kwa miaka 30 kabla ya kufariki kwa Muinjilisti huyo tarehe 5 Juni, 2021.

Ndoa yao inasemekana kukabiliwa na misukosuko na changamoto kutokana na tofauti za tamaduni zao, lakini waliweza kuzishinda changamoto hizo na kuendelea na maisha yao ya ndoa.

 Mfahamu mke wa muhubiri maarufu wa Nigeria TB Joshua

Watoto

Ndoa ya Mchungaji TB Joshua na Evelyn Joshua ilizaa matunda, kwani waliweza kubarikiwa na watoto watatu, wawili miongoni mwao wakiwa maarufu.

Kulingana na Bi Evelyne TB Joshua, mume wake, hakujali sana suala la jinsia ya watoto wake licha ya kwamba watoto wa kiume huangaliwa kwa namna ya kipekee katika utamaduni wa jamii yake.

Serah Joshua Serah, mwanae mkubwa kati ya mabinti zake watatu, ni muhitimu wa mafunzo ya sheria katika Chuo Kikuu cha masuala ya kiuchumi London School of Economics na kwa sasa anasomea Shahada yake ya uzamifu (PhD).

Alisajiliwa katika baraza la mawakili nchini Nigeria kama mwanasheria anayefanya kazi hiyo mwezi Disemba 2015.

Serah aliolewa na mwanaume wa Kitanzania mjini Arusha mwaka 2021.

Mwanae Promise pia ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha London School of Economics akisomea masomo ya mahusiano ya kimataifa na siasa.

Promise kwa sasa anasomea Shahada ya uzamili.

Mtoto wa mwisho mdogo kati ya watoto wa Evelyne hafahamiki, kwani hakuna taarifa zinazomuhusu.

Chanzo: BBC

Download Now 405