Mbosso ameendelea kuonyesha nguvu zake kimuziki kupitia EP yake ya Room Number 3, iliyotolewa rasmi Juni 13, 2025. Hadi sasa, EP hiyo imekusanya jumla ya streams milioni 121.08, na idadi hii inaendelea kuongezeka kwenye Boomplay, YouTube, Audiomack na Spotify.
Kwenye YouTube na YouTube Music, EP nzima imesikilizwa zaidi ya mara milioni 68.8. Wimbo wa Pawa pekee umevutia zaidi ya wasikilizaji au watazamaji milioni 48, na kuweka rekodi ya kuwa wimbo wa Bongo Fleva uliosikilizwa zaidi kwenye YouTube Music mwaka huu.
Kwenye Spotify, nyimbo zote 6 za EP hii zimesikilizwa jumla ya milioni 16.1, huku Boomplay ikirekodi streams milioni 30.9.
EP hii pia kwa sasa ipo nafasi nafasi ya tatu kwenye chati za Apple Music Tanzania, huku wimbo wa Pawa ukiendelea kushika nafasi ya juu kwenye chati tofauti za ndani ya Tanzania. Mafanikio haya yanaonyesha umaarufu na ukuaji na kukubalika kwa Mbosso_ kwenye biashara ya muziki.