Dr. Mpango Ataka Watu Kumuomba Mungu Msamaha Aondoe Corona

2 years ago By Nyimbo Mpya 683
Are you a music lover looking for the latest track to add to your playlist? Look no further. Get ready for an unforgettable musical experience as we present a song by Dr. Mpango Ataka Watu Kumuomba Mungu Msamaha Aondoe Corona.

Dr. Mpango Ataka Watu Kumuomba Mungu Msamaha Aondoe Corona


MAKAMU wa Rais, Dk Philip Mpango amewaomba viongozi wa dini na waumini wa dini zote kumuomba Mungu msamaha ili afukuze ugonjwa wa corona duniani ili watu wake waendelee kumtukuze na kumwabudu kwa furaha, amani na bila hofu.

Ameomba pia viongozi wa dini na Watanzania wote kuendelea kuombea nchi amani na kuwaombea viongozi wa serikali itokayo kwa Mungu.

Alitoa maombi hayo juzi wakati wa Ibada ya Misa Takatifu ya Kumbukumbu ya Mwaka mmoja tangu kufariki kwa Rais wa Awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, iliyofanyika Lupaso wilayani Masasi katika Mkoa wa Mtwara.

“Nitumie pia fursa hii kuwaomba viongozi wetu wa dini na waumini wa dini zote kumwomba Mungu msamaha ili afukuze ugonjwa huu duniani ili watu wake wamtukuze na kumwabudu kwa furaha na amani bila hofu ya corona,” alisema.

Katika hotuba yake ambayo alizungumzia mambo mbalimbali kuhusu Mkapa, Dk Mpango alisisitiza umuhimu wa kila mwananchi kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona (COVID- 19).

Alisema wataalamu wa afya wanasema kwamba awamu ya sasa ya ugonjwa huu, dalili zake haziko wazi kama zilivyokuwa awali lakini ni hatari kwani zinaweza kutuletea madhara makubwa kiafya na hata kusababisha kifo ndani ya muda mfupi zaidi.

Dk Mpango alisema ugonjwa huu si janga la kiafya pekee, bali pia la kiuchumi pia. Mbali na sekta ya afya, alisema umeathiri zaidi sekta za utalii, usafirishaji na uagizaji wa bidhaa muhimu hususani mashine na vipuri kutoka nchi za nje, vinavyohitajika katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Aliwasihi wananchi wote kuchukua tahadhari zote kama inavyoelekezwa na wataalamu wa afya ikiwa ni pamoja na kunawa mikono mara kwa mara kwa sabuni na maji tiririka, kutumia vitakasa mikono na kuvaa barakoa.

Alihimiza kuepuka misongamano ya watu isiyo ya lazima na inapowezekana, iachwe umbali wa meta moja kati ya mtu na mtu kama ilivyofanyika katika ibada hiyo iliyofanyika katika Kijiji cha Lupaso, wilayani Masasi.

Chanzo: Habari Leo

Download Now 683
Install Android App
Developer: Tanzania Tech Media
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot