Dk Mpango Ashiriki Misa Takatifu, Ataka Watu Wafanye Kazi

2 years ago By Nyimbo Mpya 936
Are you a music lover looking for the latest track to add to your playlist? Look no further. Get ready for an unforgettable musical experience as we present a song by Dk Mpango Ashiriki Misa Takatifu, Ataka Watu Wafanye Kazi.

Dk Mpango Ashiriki Misa Takatifu, Ataka Watu Wafanye Kazi


Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango ameungana na waumini wa Kanisa Ktoliki Parokia ya Mtakatifu Paulo wa Msalaba Jimbo Kuu la Dodoma kushiriki misa takatifu ya sherehe za Bikira Maria mama wa Mungu pamoja na kumshukuru Mungu kwa mwaka mpya 2022.

Makamu wa Rais amewataka watanzania kwa mwaka 2022 kufanya kazi kwa bidii kwa kuwa hata vitabu vya dini vinasisitiza juu ya kazi na Mungu huweka baraka kwa wale wafanyao kazi.

Amesema hakuna maendeleo yanayoweza kutokea pasipo kufanya kazi.

Amewaomba waumini hao kuendelea kuliombea taifa pamoja na viongozi wake ili waweze kuongozwa na hekima ya Mungu katika kuwatumikia watanzania.

Misa hiyo imeongozwa na Paroko wa parokia hiyo, Onesmo Wisi.

Akizungumza na waumini hao mara baada ya kumalizika kwa misa hiyo Dk Mpango amewasihi waumini na watanzania wote kuendelea kumshukuru Mungu kwa kuvuka salama mwaka 2021 kwa kuwa mwaka huo ulikuwa na changamoto nyingi zikiwemo za maradhi ya Covid-19.

Aidha amesema ni muhimu kutumia mvua zinazoendelea kunyeesha kupanda mazao ya muda mfupi na muda mrefu kulingana na maeneo husika.

Aliwasihi wananchi wa Dodoma pia kutumia mvua zinazoanza kunyesha kupanda miti katika maeneo yao ili kulinda mazingira pamoja na kuupendezesha mkoa wa Dodoma uliokabiliwa na upungufu wa mvua kwa muda mrefu.

Alisema wazazi wanapaswa kuwaongoza watoto wao na kuwalea katika maadili mema ikiwemo kukabiliana na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii.

Chanzo: Habari Leo

Download Now 936
Install Android App
Developer: Tanzania Tech Media
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot