DINI Zisiwe Majukwaa ya Siasa – Majaliwa

2 years ago By Nyimbo Mpya 947
Are you a music lover looking for the latest track to add to your playlist? Look no further. Get ready for an unforgettable musical experience as we present a song by DINI Zisiwe Majukwaa ya Siasa – Majaliwa.

DINI Zisiwe Majukwaa ya Siasa – Majaliwa


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa wito kwa taasisi za dini kujiepusha kutumia nyumba za ibada kama majukwaa ya kisiasa, badala yake ziendelee kushirikiana na serikali katika kujenga taifa la watu wenye hofu ya Mungu, heshima, upendo na wenye kudumisha amani na utulivu nchini.

Pia amesema serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan inaheshimu, inathamini na kutambua mchango mkubwa unaotolewa na taasisi za dini katika kujenga jamii ya wacha Mungu, wenye kutii mamlaka na sheria.

Waziri Mkuu aliyasema hayo juzi kwenye hafla ya uzinduzi wa msikiti wa Jamiu Assaliheen uliojengwa na taasisi ya Istiqaama katika Kata ya Ikwiriri, wilayani Rufiji, Pwani.

Msikiti huo una uwezo wa kutumiwa na waumini 500 kwa wakati mmoja na una vyumba vinne vya madrasa kwa ajili ya kutoa elimu ya dini na malezi mema kwa watoto.

Waziri Mkuu alisema serikali kwa upande wake itaendelea kushirikiana na taasisi zote za kidini zenye nia safi na thabiti ili kuhakikisha miradi na mipango mbalimbali ya kijamii na kiroho yenye manufaa kwa umma wa Watanzania inaendelea kutekelezwa kama ilivyokusudiwa.

“Sote ni mashahidi kuhusu mchango mkubwa unaotolewa na madhehebu au taasisi za dini katika jamii yetu. Taasisi za kidini nchini zimekuwa zikijihusisha kwa kiwango kikubwa na utoaji wa huduma za kijamii hususan elimu, maji, afya, kusaidia watu wenye uhitaji kama vile yatima na wajane sambamba na malezi na utoaji wa huduma za kiroho,” alisema.

Majaliwa alitumia fursa hiyo kuipongeza Jumuiya ya Istiqaama kwa kazi nzuri wanazozifanya nchini ikiwemo kujenga mshikamano baina ya waislamu wa madhehebu mbalimbali lakini pia baina ya waislamu na waumini wa dini nyingine.

“Hivyo basi, tuendelee kumuomba Mwenyezi Mungu atujaalie sote moyo wa subra na kujitolea katika mambo ya heri. Niwapongeze kwa kazi nzuri ya kujenga misingi mizuri ya kiroho na kimaadili kwa vijana wetu ambao ndiyo Taifa na viongozi wetu wa kesho. Jambo hili ni la msingi sana kwani ni dhahiri kuwa hakuna taifa lolote duniani linaloweza kufanikiwa bila ya kuwa na misingi imara ya kiroho na kimaadili,” alisema.

Chanzo: Habari Leo

Download Now 947
Install Android App
Developer: Tanzania Tech Media
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot