Country Wizzy aondoka Konde Gang na kujiunga Roof Top tena — citiMuzik

4 months ago 496
Country Wizzy aondoka Konde Gang na kujiunga Roof Top tena — citiMuzik, download Nyimbo Mpya. Stream and Download Country Wizzy aondoka Konde Gang na kujiunga Roof Top tena — citiMuzik on Nyimbo Mpya.

Country Wizzy aondoka Konde Gang na kujiunga Roof Top tena

Country Wizzy aondoka Konde Gang na kujiunga Roof Top tena

Lebo muziki ya Konde Music Worldwide inayoongozwa na Msanii wa Bongo Fleva, Harmonize, imepata pigo baada ya kuondokowe na Msanii wao pendwa, Country Wizzy.

RELATED: Country Wizzy – Watoto Ft Harmonize (Prod. S2kizzy)

Lebo hiyo imetangaza kukamilika kwa mkataba wake na msanii maarufu Country Wizzy, ambaye hakutaka tena kuendelea kufanya kazi chini ya lebo hiyo.

Kupitia chapisho liloliwekwa katika mtandao wa Instagram wa Konde Music Worldwide iliwajulisha wafuasi wake kuwa mkataba huo ulikamilika mnamo tarehe nane, mwezi wa huu wa Januari.

“Taarifa: Mkataba kati ya Konde Music Worldwide na @countrywizzy_tz umemalizika hii leo tar 8 January 2022. Kuanzia leo Country Wizzy atakuwa msanii anaejitegemea baada ya kufikia makubaliano ya pande zote mbili.

Konde Music Worldwide inamtakia kila lenye kheri Country Wizzy kwenye career yake ya music pamoja na maisha kwa ujumla. All the best Wizzy,” – tangazo kutoka Konde Music Worldwide lilisomeka.

Also, check more tracks from Harmonize;

Download Now 496