Chidinma Ekile Aendelea Kuchapa Kazi ya Uinjilisti

1 year ago 305
Chidinma Ekile Aendelea Kuchapa Kazi ya Uinjilisti. Get ready for an unforgettable musical experience as we present new song by Chidinma Ekile Aendelea Kuchapa Kazi ya Uinjilisti Stream and download below.

Chidinma Ekile Aendelea Kuchapa Kazi ya Uinjilisti Song


Mwanamuziki maarufu kutoka Nigeria Chidinma Ekile alitangaza hivi karibuni kwamba ameacha kufanya muziki wa kidunia na atakuwa akifanya zaidi sana muziki za injili.

Kwenye video kadhaa ambazo ameposti kwenye mitandao ya kijamii, Chidinma anaonekana akihubiri injili hata kwa walevi kwenye vilabu. Mwanamuziki huyo ameingia katika wokovu kwa kishindo na ana imani kwamba atabadilisha maisha ya wengi.

Kwenye mtandao wa Instagram Ekile aliwahakikishia wafuasi wake kwamba amebadilisha maisha yake na amefungua ukurasa mpya,” Mimi sasa ni soja wa zama za mwisho, ujumbe wangu ni Yesu.”

Katika kupekua baadhi ya kurasa zake mitandaoni imebainika kwamba msanii huyo anazitumia kurasa hizo kuhubiri injili na siku ya Jumanne ameitenga kuwa ya kutoa ushuhuda.

Chidinma ametambulika kwa nyimbo kadhaa ikiwemo Kedike na inasemekana alianza kufanya muziki akiwa na umri wa miaka 19.

Chidinma, 30, alikuwa mshindi wa shindano la muziki la Project Fame West Africa mwaka wa 2010, hapo ndipo alipopata umaarufu zaidi katika ulingo wa muziki.

Msanii huyo alitangaza kwamba atakuwa akifanya muziki wa injili pindi alipotimia umri wa miaka 30, habari ambazo zilipokelewa na hisia tofauti miongoni mwa mashabiki wake. Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe?

Chanzo: TUKO

Download Now 305