Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, lampongeza Rais Samia Suluhu

2 years ago By Nyimbo Mpya 546
Are you a music lover looking for the latest track to add to your playlist? Look no further. Get ready for an unforgettable musical experience as we present a song by Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, lampongeza Rais Samia Suluhu.

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, lampongeza Rais Samia Suluhu


Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, TEC, hivi karibuni, limempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kupokea majukumu ya urais wa nchi ya Tanzania, kuwa Mwanamke wa kwanza kuiongoza Tanzania, kuendesha kipindi cha mpito kwa serikali ya awamu ya tano kwenda awamu ya sita kwa utulivu na amani.

Katika pongezi hizo zilizosomwa mbele ya Rais Samia na Askofu mkuu Gervas Nyaisonga, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania ambalo limempongeza pia Rais Samia kwa kuendeleza na kuongeza mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Virusi vya Korona, UVIKO-19 pamoja na kuimarisha utetezi na ulinzi wa haki msingi za binadamu kwa njia mbalimbali.

“Tunamshukuru Mungu kukubali wewe kuwa Kiongozi wa Taifa letu na tunakuombea Hekima, Afya na Mshikamano, Mungu akuwezeshe kutimiza majukumu yako vema na uweze kukidhi matarajio ya watanzania wote uliokabidhiwa” nukuu ya sehemu mojawapo ya salamu hizo za pongezi.

Mkutano kati ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ulifanyika katika Ukumbi wa Baraza la Maaskofu Katoliki uliopo Makao Makuu ya Baraza, Kurasini, Jimbo Kuu la Dar es Salaam.

Askofu Mkuu Nyaisonga amemhakikishia Rais Samia kuwa Baraza litatoa ushirikiano kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika masuala yote yenye ustawi, maendeleo na mafao ya watanzania, kuwa Kanisa Katoliki linajishughulisha na ustawi wa mtu mmoja mmoja na ustawi wa jamii, Kanisa linajishughulisha kumstawisha mwanadamu kiroho na kimwili. Kwa vile ni jukumu la Kanisa kumkomboa mwanadamu dhidi ya utumwa wa aina yoyote ile jambo ambalo ni msingi wa uwepo wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania.

Salamu za Baraza la Maaskofu Nchini Tanzania zimekwenda sanjari na ombi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kurejea nia yake ya awali ya kurekebisha sera mbalimbali katika sekta ya Elimu ili vyuo na taasisi za elimu ya juu zinazosimamiwa na Kanisa ili ziweze kutoa elimu kwa watu wenye hali duni ya maisha hususani vijijini liweze kufanikiwa.

Download Now 546
Install Android App
Developer: Tanzania Tech Media
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot