Tip of the Day - Music
The annual Ngoma festivals, held in different regions, showcase the rich diversity of Tanzanian music, bringing together traditional groups and modern artists in a celebration of dance and sound.
Stamina ft Mkwawa – Umaskini Niache mp3 download, Tanzanian heavyweight Hip Hop recording artist and a key member of Rostam group, Stamina came through with another his 2022 single titled Umasikini Niache from his Album Paradiso. Enjoy, Nyimbo za Stamina
Stamina Umasikini Niache Lyrics
Mmh Wamemchokoza tena…
Wamemchokoza Bea!!!!
Umaskini niachee.. (Eeh Eeh Eeh)
Umaskini naiache.. (Eeh Eeh Eeh)
Ulimuondoa mama kipindi yupo hoi anaumwa
Kapoteza uhai kisa pesa ya matibabu hakuna
We ndo sababu ya kuvunja ndoa ya fatuma
Mumewe mambo mazito hujampa pesa umemchuna
Niache niende bwana, Nimechoshwa na maisha ya huku Sitimbi
Unazani sitaman kupiga picha kidimbwi
Nizungishe wapambe mezani tungi jing
mixer kuagiza vinywaji vijazwe na cheche nyingi
Umeniganda Asee, umeniganda kama Ruba,
Hivi we ni jinsia Gani, hivi ni pisi ama Mjuba.
Unanichanganya una mda nautaman msuba,
unanzeesha unanikonda sa si unipe tu hizo fuba.
We ndo sababu ya dada zangu wakae Kona wanajiuza,
Na kaka zangu wawe wezi huko buza,
Na mama zangu wakeshe kuuza vitumbua
Unawatesa Baba zangu kuwazungusha kwenye Jua..!
Usione tabasamu usoni, moyoni mm sina Furaha
usio napendeza nje, ndani mi nakosa na njaa
Umaskini niache (Niache, niache)
Umaskini niache (Niache, niache)
Nimesoma kidumu ufagio kayumbe ndo ninakoweza,
hivi unazan sitaman watoto wangu wasome Feza?
Daily kwa mganga napiga manyanga, nazi njia panda ili mradi tu niweze kuupata hu mkwanja
Nikuulize? nikiwa tajiri inakuuma nini..
Au ninavyoitwa mbahili kiongozi unapata nini
Kaka zangu boda boda nao utawapa pesa lini,
Asee tumechoka kubeti tunaliwa kama nini.
Kwenye mapenzi, wengi tupo tu ilimradi ukiitwa mpenzi na hauna pesa we ni mpenzi mtizamaji.
Au unafurahi nikiitwa dume suruali, Dume nisiye na gari Dume nisiye na maisha ya Ufahari.
Mbona wezangu unawapa marose rose maprado, Mi nikiendesha ujue naharisha,
Mbona kwangu mambo bado.
Inatosha Asee hembu niache niende zangu,
Nipate utajiri nikakae na maboss wezangu.
Usione tabasamu usoni, moyoni mm sina Furaha
usio napendeza nje, ndani mi nakosa na njaa
Umaskini niache (Niache, niache)
Umaskini niache (Niache, niache)
watoto washangazi bado niwahudumu wa Bar,
Hawapendi wanachofanya, sema ndo ivo tu wana njaa
Na mjomba wangu bado ni mkata mkaa, mtoto wake fundi muashi fundi mjenzi wa majengo ya mtaa
Hivi kwanini kazi ngumu zote za sisi maskini, unatuona Power mabula ee Daa hivi kwanini
Maisha wanayoishi yote tuanayaunda sisi,
Mijengo magari mpaka hayo maofisi.
Nachukia nikiona sura ya mbunge wangu nawaambia haki ya nani nimepoteza kura yangu,
Anasinzia Bungeni hatetei maisha yangu bora peke yangu, Mimi pekee nafuu kulala….
Usione tabasamu usoni, moyoni mm sina Furaha
usio napendeza nje, ndani mi nakosa na njaa
Umaskini niache (Niache, niache)
Umaskini niache (Niache, niache)
Umaskini niachee..
Nimekuchoka.. (nimeku…choka!)
Nimekuchoka..
Nimekuchoka umaskini..
Nimeku…chokaa…