Askofu Ruwai’chi Aagiza Mapadri Kupata Chanjo Dhidi ya Uviko-19

2 years ago By Askofu Ruwai’chi Aagiza Mapadri Kupata Chanjo Dhidi ya Uviko 700
Are you a music lover looking for the latest track to add to your playlist? Look no further. Get ready for an unforgettable musical experience as we present a song by Askofu Ruwai’chi Aagiza Mapadri Kupata Chanjo Dhidi ya Uviko9.

Askofu Ruwai’chi Aagiza Mapadri Kupata Chanjo Dhidi ya Uviko19


Askofu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mhashamu Yuda Tadheus Ruwai’chi ameagiza mapadri wote wa jimbo hilo kupata chanjo dhidi ya Uviko 19 kwa kuwa ugonjwa huo unaumiza na kuondoa uhai.

Ametoa agizo hilo leo Jumanne Agosti 24, 2021 katika adhimisho la Misa Takatifu ya kumuombea Padri Paul Haule aliyekuwa Paroko Msaidizi katika Parokia ya Mtakatifu Petro na Mkurugenzi wa Tumaini Media.

Ruwai’chi amesema mwaka 2020 wakati wa awamu ya kwanza ya janga la Uviko-19 watu walimuomba Mungu ajaalie kupatikana kwa chanjo, ambayo sasa imepatikana.

“Tulimuomba Mungu ajaalie kupatikana kwa chanjo sasa imepatikana badala ya kutumika watu wameingia katika malumbano ya kusema haya na yale dhidi ya chanjo,” amesema.

“Tusingojee hadi mambo haya yatutinge, tutumie vizuri fursa alizotupa Mungu kujikinga na kujihami na kwa sababu hiyo, sijui ni mapdri wangapi ambao mmeshachanjwa, lakini leo naomba nitoe agizo, kila padre akachanjwe, kila padre akachanjwe, tusifanye utoto, tusifanye lelemama, hii uviko 19 haina mjomba na shemeji na inatuondolea uhai,” amesema Ruwai’chi

Amesema ni utashi wa Mungu kwa watu wawe hai na kuwa na uhai tele hivyo ni vyema kuujali uhai waliopewa.

“Tujihami na tuendelee kumuomba Mungu, atuhurumie na tujihami na atuondolee hili janga,” amesema Ruwai’chi.

Chanzo: Mwananchi

Download Now 700
Install Android App
Developer: Tanzania Tech Media
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot