Askofu Ranwell Mwenisongole Kuzikwa Leo, Mtoto Wake Afunguka

2 years ago By Nyimbo Mpya 1.2K
Are you a music lover looking for the latest track to add to your playlist? Look no further. Get ready for an unforgettable musical experience as we present a song by Askofu Ranwell Mwenisongole Kuzikwa Leo, Mtoto Wake Afunguka.

Askofu Ranwell Mwenisongole Kuzikwa Leo, Mtoto Wake Afunguka


Wakati mwili wa Askofu Mkuu Mstaafu wa Tanzania Assembles of God (TAG) Dk Ranwell Mwenisongole ukitarajiwa kuzikwa leo Vwawa mkoani Songwe, mwanawe ambaye ni mbunge wa Mbozi, George Mwanisongole amesema baba yake ana mchango mkubwa katika safari yake ya kisiasa.

Profesa Mwanisongole alifariki dunia Jumamosi Desemba 25, 2021 katika hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa ibada ya mazishi katika kanisa alilokuwa akihudumu na alilolianzisha marehemu baba yake, George alisema wakati anagombea ubunge baba yake alimchangia fedha nyingi na baada ya kushinda alidhani ataambiwa amrudishie lakini alimpa tena zawadi ya gari.

Alisema baba yake alikuwa kama kampeni meneja wake kwa kuwa alipanda katika majukwaa ya siasa kuhutubia na kumuombea kura kwa wananchi na alikaa Mbozi kwa zaidi ya mwezi akifanya kazi hiyo.

George alisema siku ambayo baba yake alifariki dunia alimpigia simu saa 4 usiku na kumuuliza yuko wapi na alimjibu kuwa yuko Dodoma.

Alisema baba yake alimueleza kuwa yupo kwenye vita kali sana na kumtaka aende kumuona (Dar es Salaam) na yeye George alimuahidi angefanya hivyo kesho yake (siku ya Krismasi) lakini hakuitimiza kwa kuwa baba yake alifariki.

Alisema mama yake, Irene alipata nafasi ya kumuaga na mumewe kwa kuwa aliamshwa na marehemu aliyemuomba amfunike kwa sababu hajisikii vizuri.

Alisema wakati akifunikwa alimuambia mkewe kuwa anamuacha, jambo lililomfanya mama yake kuonyesha kutoelewa na kauli hiyo kutamkwa mara ya pili kuwa nakuacha.

“Mama akaanza kubishana naye kuwa usiseme hivyo, we bado utabaki. Basi wakaanza kuomba wote wawili na walipomaliza mama akamfunika akifikiri amelala, lakini ndiyo ikawa safari.”

Akitoa salamu kwa niaba ya wabunge, Juliana Shonza alimtaka George kutokuwa na wasiwasi juu ya nani atamsaidia katika kampeni za uchaguzi mwaka 2025, huku akimuahidi kuwa watakuwa naye.

“Nikutie moyo kuwa sisi ndugu zako wa Mbozi tupo tutasimama pamoja nawewe. Nimejifunza kwa baba yetu huyu ambaye ametangulia mbele za haki na mimi kama kiongozi kijana ni kuandaa watoto wetu kuwa viongozi.”

Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Profesa Elisante Ole Gabriel alisema viongozi wa dini wana nafasi kubwa katika kuhubiri haki, kwani watu wakiifahamu kweli nayo kweli itawaweka huru.

“Askofu Mwanisongole alihubiri kweli, hakutaka mchezo, alikuwa amenyooka. Mpaka sasa siamini kama amefariki,” alisema.

Chanzo: Mwananchi

Download Now 1.2K
Install Android App
Developer: Tanzania Tech Media
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot