Askofu Malasusa Akemea Wachungaji Kupenda Utajiri wa Haraka

2 years ago By Nyimbo Mpya 732
Are you a music lover looking for the latest track to add to your playlist? Look no further. Get ready for an unforgettable musical experience as we present a song by Askofu Malasusa Akemea Wachungaji Kupenda Utajiri wa Haraka.

Askofu Malasusa Akemea Wachungaji Kupenda Utajiri wa Haraka


Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani (DMP), Dk Alex Malasusa amewaasa wachungaji kutopenda utajiri wa haraka kwa kile alichosema ni ‘kiatu’ kibaya na hatari.

Aidha, amebainisha mambo mengine mabaya aliyoyarejea kama ‘viatu’ ambayo wachungaji wanapaswa wayaepuke ni kiburi cha uzima na kufanya kazi kwa mazoea, huku pia akikemea tabia ya baadhi ya wachungaji kupenda kukuza majina yao badala ya kutukuza jina la Mungu.

Askofu Dk Malasusa alisema hayo katika ibada ya kuwabariki wachungaji sita wa Dayosisi hiyo iliyofanyika jana katika Kanisa Kuu la Azania Front, Dar es Salaam.

“Kuna kiatu sasa ndio cha wakati, cha kupenda fedha na mali. Zamani wachungaji waliogopa kutambulisha mali zao ila leo tunataja, wachungaji wa sasa tunataka utajiri wa harakaharaka, kiatu hiki ni kibaya na hatari, vua kiatu hicho. Mchungaji anaanza kazi Jumatatu, Ijumaa anataka awe tajiri.”

“Sisemi tuwe masikini, ila tusitangulize fedha kama ndio kila kitu, unatetemeka kwa kupenda fedha,” alisema.

Askofu Dk Malasusa alisema kazi ya uchungaji ni yenye baraka na heshima na Mungu anataka iendeshwe kwa utaratibu.

“Vua viatu vyako, kuna viatu vingi Mungu anataka tuvivue, kimoja kibaya ni kiburi cha uzima ni kitu kibaya sana, Mungu akikupa kidogo tu kama punje ya haradali unajinyanyua. Nimeona wachungaji wengi walianza vizuri, kiburi kikainuka hata usharika ulianza chini ukainuka, kiburi kikajaa,” alisema.

Alisema imefikia mahali baadhi ya waumini wanamwamini mchungaji kuliko Yesu, kiasi kwamba hata huyo mchungaji akihamishwa wanahoji na kusema hivyo vyote ni ‘viatu vibaya ambavyo vinapaswa kuvuliwa.

Kuhusu kiatu cha mazoea, alisema kimewabana wengi. “Hiki nacho kinatubana wengi, tunajiita senior, tena Senior Pastor, tunaacha kumtafuta Mungu, baadhi ya watumishi kabla ya kubarikiwa kuwa wachungaji walikuwa wazuri, lakini baada ya kubarikiwa leo wananyanyua mabega,” alisema Dk Malasusa.

Alisema Mungu anatoa ahadi kwa wanadamu ya kuwafanya taifa kubwa na kuwapa baraka endapo tu watakuwa watii kwenye neno lake.

“Siku hizi watu wanafanya bidii kukuza majina yao, tukuze jina la Yesu. Lakini pia Mungu anasema nitalikuza jina lako, hivyo usifanye bidii wewe mwenyewe kulikuza jina lako, bali fanya bidii kumtii Mungu, naye atakuza jina lako,” alisema.

Alisema watu wanapenda kujikuza majina yao na hivyo kukosa baraka kwa Mungu na kuwataka wajifunze kwa Ibrahimu Baba wa Imani ambaye alikuwa mtii na Mungu akampa Baraka, hivyo hata leo wanadamu wakitiii watapata baraka kuanzia kwenye familia hadi ofisini.

Katika hatua nyingine, Askofu Dk Malasuasa alisema wahubiri wengi wanahubiri jinsi ya kubarikiwa, lakini hawawakumbushi waumini kuacha dhambi.

Alisema waajiriwa wa kanisa ni wengi kwa maana ya wachungaji, wainjilisti na wengine, lakini wafanyaokazi kwa kusudi la Mungu ni wachache.

Akitoa salamu za Kanisa la KKKT-Tanzania, Katibu Mkuu wa kanisa hilo, Robert Kitundu aliwataka wachungaji kuwa waaminifu na kuwataka waumini na kanisa kwa ujumla kuwasaidia na kuwapa ushirikiano ili watende kazi ya Mungu kwa utii.

Wachungaji sita waliobarikiwa katika ibada hiyo ni, Godwin Amirimere, Elizabeth Mdoe, Eliabu Masaki, Jane Kamugisha, Steven Kibiki na Hossiana Mchome.

Chanzo: Habari Leo

Download Now 732
Install Android App
Developer: Tanzania Tech Media
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot