Askofu Gwajima: Niko tayari kuachia ubunge kuliko kuchanjwa

2 years ago By Nyimbo Mpya 968
Are you a music lover looking for the latest track to add to your playlist? Look no further. Get ready for an unforgettable musical experience as we present a song by Askofu Gwajima: Niko tayari kuachia ubunge kuliko kuchanjwa.

Askofu Gwajima: Niko tayari kuachia ubunge kuliko kuchanjwa


Askofu wa kanisa la Ufufuo na Uzima na Mbunge wa jimbo la Kawe Josephat Gwajima ameendelea na msimamo wake wa yeye na waumini wake kutochanjwa, akieleza kuwa Bunge likilazimisha hatochanjwa.

Hata hivyo, ufafanuzi uliotolewa na Ofisi ya Bunge hivi karibuni umesema hakuna mbunge aliyelazimishwa kupata chanjo hiyo.

Akizungumza katika ibada yake leo Agosti 15, Gwajima amesema chanjo hiyo inayoendelea kutolewa nchini hazijafanyiwa utafiti wa kina kubaini madhara yake kwa wanaochanjwa na vizazi vijavyo.

“Wanaotaka nifukuzwe CCM watumie akili, kwa mfano tukichanja wote halafu kufikia 2025 watu wako hoi tunapigaje kampeni, bora wengine tubaki tusaidie kutetea chama chetu,”.

“Kulikuwa na twitter inasambaa kwamba wabunge wote wachanjwe, baadae Ofisi ya Bunge ikakanusha nikasema hata ingekuwa kweli mie nisingechanjwa, ni heri kurudi hapa nyumbani, ubunge ni mzuri una heshima unasaidia wananchi lakini kunichanja hapana,” amesema askofu Gwajima.

Hata hivyo amesema hapingi chanjo kwa ujumla wake:  “Sipingi chanjo ila hii haijafanyiwa tafiti za kutosha kwa maana hiyo nasema hapa hajachwi mtu. Mimi sio adui yenu nalinda kizazi chenu kijacho na Tanzania yetu ijayo kwa nguvu zangu zote.”

Chanzo: Mwananchi

Download Now 968
Install Android App
Developer: Tanzania Tech Media
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot