Askofu Desmond Tutu Azikwa Afrika Kusini

2 years ago By Nyimbo Mpya 813
Are you a music lover looking for the latest track to add to your playlist? Look no further. Get ready for an unforgettable musical experience as we present a song by Askofu Desmond Tutu Azikwa Afrika Kusini.

Askofu Desmond Tutu Azikwa Afrika Kusini


Maziko ya Askofu Desmond Tutu (90), mwanaharakati na mpinga ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini yamefanyika katika Kanisa Kuu la Anglikana la Mtakatifu George mjini Cape Town, Afrika Kusini.

Wananchi wa Afrika Kusini wamekuwa katika maombolezo kwa tarkibani siku sita sasa huku wakipata nafasi ya siku mbili kuaga mwili wa kiongozi huyo ambaye pia ni mshindi wa tuzo ya Amani ya Nobel.

Ibada hiyo ya maziko ilifanya na kuhudhuriwa pia na Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa ambaye alimuelezea Askofu Tutu kama alama ya maadili katika jamii isiyofutika.

Ibada ya mazishi hayo ilihudhuriwa na maaskofu mbalimbali, mapadri, wachungaji na watumishi wengine wa dini wakiwemo ndugu jamaa na marafiki.

Katika salamu zake za rambirambi, Rais Ramaphosa alimuelezea Askofu Tutu kuwa hata baada ya taifa hilo kupata uhuru na kuwa na demokrasia aliendelea kuwa mwadilifu na mwenye heshima.

Baada ya salamu zake hizo Rais Ramaphosa alitoa bendera na kumpa mjane wa Tutu aitwaye Leah kuonesha kuheshimu mchango wake kwa taifa hilo.

Hata hivyo ibada hiyo ilihudhuriwa na waombolezaji wasiozidi 100 ikiwa ni hatua ya kupambana na mlipuko wa maradhi ya Covid-19.

Askofu Tutu alifariki dunia Desemba 26, mwaka huu nchini humo baada ya kuugua saratani kwa muda mrefu.

Juzi, mwili wake uliwasili katika Kanisa Kuu la Mtakatifu George mjini hapa kwa ajili ya wananchi kutoa heshima za mwisho, kwa muda wa siku mbili na jana kuzikwa rasmi.

Chanzo Habari Leo

Download Now 813
Install Android App
Developer: Tanzania Tech Media
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot