Askofu Aihimiza Waumini Kufanya Kazi

1 year ago 459
Are you a music lover looking for the latest track to add to your playlist? Look no further. Get ready for an unforgettable musical experience as we present a song by Askofu Aihimiza Waumini Kufanya Kazi.

Askofu Aihimiza Waumini Kufanya Kazi


ASKOFU wa Kanisa la Anglikana Tanzania Dayosisi ya Central Tanganyika, Dk. Dickson Chilongani, amewataka waumini wa kanisa hilo kujishughulisha na ujasiriamali na vikundi vya vikoba ili kuondokana na umaskini.

Dk. Chilongania alibainisha hayo jana jijini Dodoma alipokuwa akifunga mafunzo ya vikoba na ujasiriamali kwa wanawake wa Ushirika wa Mama wa Kikristo wa Kanisa Anglikana Tanzania (UMAKI).

Alisema mafunzo ya ujasiriamali ni muhimu kwa wakati huu kwa waumini wa kanisa hilo nchini ili kuondokana na umaskini katika kaya zao.

“Kuna watu wanaishi kana kwamba Yesu anarudi kesho. Mtu ana maisha magumu lakini hana shamba wala hajishughulishi na ujasiriamali watoto wanapata shida hata kwenda shule ni shida.

“Tunapaswa kubadilika, walipokuja wamisionari kuleta dini walitufanya kuona kuwa mtu ukishaokoka basi wewe huna sababu ya kushughulika na ujasiriamali au uzalishaji mali lakini wao walipokuja walifanya kazi na walichuma mali hapa hapa kwetu na kwenda nazo kwao na sisi tukaendelea kuwategemea wao,” alisema.

Dk. Chilongani alisema kinachotakiwa hivi sasa si waumini kupatiwa msaada wa fedha bali ni kuwezeshwa ili kubadili mitizamo yao.

“Hata Yesu mwenyewe anatusisitiza kufanya ujasiriamali. Walikuja wamisionari waliotuaminisha kuwa hatuna sababu ya kufanya kazi lakini tulipoisoma Biblia wenyewe tumebaini kuwa kufanya kazi ni jambo la lazima. Tusiwe kama yule aliyepewa talanta moja akaichimbia chini bali tuzalishe zaidi kwa kile tulicho nacho,” alisema.

Pia alisema Watanzania wanaweza kutumia fursa pamoja na rasilimali zilizopo nchini ili kujikwamua kiuchumi badala ya kuendelea kutegemea misaada.

Dk. Chilongani alisema kinachotakiwa hivi sasa si waumini kupatiwa msaada wa fedha bali ni kuwezeshwa ili kubadili mitizamo yao.

“Hata Yesu mwenyewe anatusisitiza kufanya ujasiriamali. Walikuja wamisionari waliotuaminisha kuwa hatuna sababu ya kufanya kazi lakini tulipoisoma Biblia wenyewe tumebaini kuwa kufanya kazi ni jambo la lazima. Tusiwe kama yule aliyepewa talanta moja akaichimbia chini bali tuzalishe zaidi kwa kile tulicho nacho,” alisema.

“Tukifanikiwa kuimarisha maisha ya waumini wetu hata kanisa linatakuwa imara lakini kama maisha ya waumini wetu yataendelea kuwa duni, basi hata huduma ya kanisa itakuwa duni.

“Hatujui Yesu atarudi lini lakini inashangaza watu wanaoishi kama Yesu anarudi kesho. Hawafanyi kazi wala hawana shughuli yoyote ile ya kujipatia kipato. Lazima tubadilishe mitizamo yetu na viongozi wa dini tusione aibu kufundisha hivyo kwani ipo kwenye Biblia,” alisisitiza.

Aliongeza kuwa kwa wakati huu semina za ujasiriamali na vikundi vya vikoba kwa waumini ni muhimu kwa sababu kanisa bila fedha haliwezi kuendelea.

Kadhalika aliagiza viongozi wa mitaa yote zilizoko chini ya dayosisi hiyo, kuhakikisha wanawekeza miradi mbalimbali ambayo wataitumia kama vitega uchumi.

“Lazima kila Parish (mtaa) kuwa na mradi hata mmoja kila eneo nataka kuwa na mradi kama fremu za maduka au nini lakini kuwapo na mradi wa kitega uchumi cha kanisa,” alisema.

Mratibu wa UMAKI Kanisa Anglikana Tanzania, Magreth Ndonde, alisema mafunzo hayo yametolewa kwa siku tano yakijumuisha zaidi ya washiriki 40.

Chanzo: IPP Media

Download Now 459